Kwaufupi Wataalamu wa lugha wameandika kuhusu lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa na lugha rasmi inayokadiriwa kutumiwa na watu wapatao zaidi ya milioni 60 duniani kote. Tambua kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha kamili na wala si lugha chotara kwa maana ya mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha ya Kibantu kama watu wengi wanavyodhani. Endelea kujifunza juu ya asili na chimbuko la lugha ya Kiswahili. Wataalamu wa lugha wameandika kuhusu lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa na lugha rasmi inayokadiriwa kutumiwa na watu wapatao zaidi ya milioni 60 duniani kote. Hutumika katika nchi za Afrika Mashariki na Kati kama Tanzania, Kenya, Uganda na katika eneo la mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Vilevile katika nchi za Burundi, Rwanda, Msumbiji, Zambia, Comoro na Malawi. Kiswahili kinazungumzwa pia katika nchi za Uarabuni kama Dubai, Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Yemen, Dubai, n.k. Kwa kipindi cha miaka zaidi ya miaka elfu moja, ...