Serikali ya Tanzania yashusha tozo za miamala ya fedha kwa simu kwa asilimi 30
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Lameck Nchemba akisaini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kielektroniki za Kutuma na Kutoa Fedha kwa Mwaka 2021, marekebisho hayo yamepunguza viwango vya tozo za miamala hiyo kwa asilimia 30, jijini Dodoma. Picha| Wizara ya Fedha na Mipango. Watoa huduma nao wamekubali kushusha tozo wanazotoza baina ya mtandao na mtandao kwa kwa asilimia 10. Viwango vipya kutolewa Septemba Mosi, 2021. Dar es Salaam. Huenda Watanzania watapata ahueni baada ya Serikali kufanya mabadiliko katika tozo za miamala ya fedha inayofanyika kwa njia ya simu na kupunguza kwa asilimia 30. Viwango hivyo vimepungua baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba leo Agosti 31, 2021, ametia saini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kieletroniki za Kutuma na Kutoa Fedha za Mwaka 2021. Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja amesema pia Serikali imefanya majadiliano na watoa huduma za simu ambao nao wameridhia kupunguza viwan...