Baadhi wamesema wanawake waachwe wafanye wanachokitaka licha ya kuona kuwa ni kiashiria cha kutokujiamini. Kwa wanaume, kuwa na nywele asilia ni kuukubali uzuri wako na kujiamini. Hata hivyo, hayo ni maoni binafsi kutoka kwa wadau. Dar es Salaam. “Tangu niwe na mpenzi wangu, niseme ukweli tu kuwa sijawahi kuona nywele zake. Karibia kila wiki anakua na nywele mpya, leo rasta, kesho wigi, sijawahi kushika kichwa chake nikakutana na nywele zake, ” anasema Kennedy Bundala mkazi wa Morogoro. Katika mfululizo wa makala zilizopita tulielezea mambo mbalimbali yanayohusu nywele asilia ikiwemo namna ya kuzitunza na madhara kwa wanaotengeneza nywele za dawa. Hata hivyo, ni mara chache sana kusikia hisia au kuwaona wanaume wakijadili masuala ya nywele za wanawake kwa kina. Je, wanaume wanawaza nini juu ya nywele za Wanawake ambao ni wake, wapenzi, mama na hata dada zao? Bundala, ambaye amekuwa na mpenzi wake kwa mwaka mmoja na nusu sasa bila mafanikio ya kuwahi kuziona ...