Posts

Showing posts from July, 2020

Live : MISA YA KUAGA MWILI WA HAYATI BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Image
Tazama Matangazo ya moja kwa moja Misa ya Kuaga mwili wa Hayati Benjamin William Mkapa. Usikubali kupitwa na habari.. Tazama Matangazo ya moja kwa moja Misa ya Kuaga mwili wa Hayati Benjamin William Mkapa.

Season: BAGANI 1-50

Image
imetafsiriwa. Bagani ep1 Bagani ep2 Bagani ep3 Bagani ep4 Bagani ep5 Bagani ep6 Bagani ep7 Bagani ep8 Bagani ep9 Bagani ep10 Bagani ep11 Bagani ep12 Bagani ep13 Bagani ep14 Bagani ep15 Bagani ep16 Bagani ep17 Bagani ep18 Bagani ep19 Bagani ep20 Bagani ep21 Bagani ep22 Bagani ep23 Bagani ep24 Bagani ep25 Bagani ep26 Bagani ep27 Bagani ep28 Bagani ep29 Bagani ep30 Bagani ep31 Bagani ep32 Bagani ep33 Bagani ep34 Bagani ep35 Bagani ep36 Bagani ep37 Bagani ep38 Bagani ep39 Bagani ep40 Bagani ep41 Bagani ep42 Bagani ep43 Bagani ep44 Bagani ep45 Bagani ep46 Bagani ep47 Bagani ep48 Bagani ep49 Bagani ep50 MAELEZO ZAIDI UNAWEZA

Madhara ya kukaa na mkojo kwa muda mrefu

Image
Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature’s call. Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini, akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili. Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo umenibana kweli, ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi ndivyo watu wengi wanafanya. Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia, kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo, mkojo unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa. Kibofu cha mkojo kimezunguk...

Filamu ya Fatal Affair: Kiboko kwa wachepukaji

Image
David na Ellie wanaonjeshana penzi walilopeana miaka 20 iliyopita lakini linaingia doa hata kabla halijanoga. Picha|Mtandao. Inamuhusu mwanadada Ellie ambaye alichepuka mara moja tu na kujikuta akiwindwa na mchepuko wake. Hofu inatanda pale mume wake anapoanza kupata mashaka kama Ellie yupo sawa. Visa vitimbi na sintofahamu za hapa na pale, ni sehemu tu ya filamu hii ya saa moja na nusu. Dar es Salaam.  Hapa ndipo chozi linapoanza kudondoka. Pale unapochepuka na mchepuko ukakolea na mahaba yako! Mke na mama wa mtoto mmoja, Ellie (Nia Long) anajikuta kwenye njiapanda baada ya kuchepuka kwa usiku mmoja tu na kujikuta akicheza mchezo wa kifaranga na kicheche. Licha ya kuwa safari ya ukumbusho na mchepuko huyo haikufika “Galilaya”, haha! Wakubwa wameelewa, bado haikuwa rahisi kwa David (Omar Epps) kusahau mahaba mazito aliyopata kwa mwanamama Ellie. Safari ilianza hivi… “Ellie,”aliita David baada ya kumuona mrembo ambaye alioneka kuwa na historia naye ya muda mr...

Google kuwalinda wanaofuatiliwa na wapenzi wao mtandaoni

Inafanya mabadiliko ya sera yake kuzuia matangazo ya programu zinazofuatilia watu mtandaoni bila ridhaa yao.  Yasema kila mtu ana uhuru wa kutumia intaneti bila kuingiliwa.  Huenda ikawasaidia watu waliopo kwenye mahusiano kufurahia haki ya faragha mtandaoni.  Ikiwa wewe ni miongoni mwa watu ambao wanaogopa kufanya vitu kwa uhuru ukiwa mtandaoni kwa sababu tu unahofia kuna watu wanakufuatilia au wanaingilia mawasiliano yako, sasa ondoa shaka hiyo.  Kampuni ya teknolojia ya Google imetangaza kuiboresha  sera yake ya matangazo  ili kudhibiti matangazo yote ya programu za bidhaa na huduma ambazo zinahimiza kuwafuatilia watu mtandaoni bila ridhaa yao. Kampuni hiyo inayotoa huduma ya watu kutafuta vitu mtandaoni, imesema kila mtu ana haki ya faragha kwa anayoyafanya mtandaoni bila kuingiliwa na mtu yoyote.  Imesema miongoni mwa matangazo ya bidhaa na huduma hizo zitakazozuiliwa ni pamoja programu zinazotumika na watu waliopo kwenye mahusian...

SIMBA SC YAITAFUNA YANGA UWANJA WA TAIFA...YAITWANGA 4 - 1

Image
Kiungo wa timu ya Simba, Gerson Fraga akishangilia kwa kunyoosha mikono juu baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza. TIMU ya Simba SC leo imefanikiwa kusonga mbele na kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) maarufu kama Kombe la FA, baada ya kuwachapa watani wao wa jadi, Yanga SC kwa mabao 4-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa leo saa 11 jioni katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba wamengia kwa nguvu kubwa katika mchezo huo wakihitaji kulipiza kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu Machi, mwaka huu, ambapo wameutawala mchezo huo wakitandika kandanda safi na kupoteza matumaini ya wapinzani wao kupata ushindi. Mabao ya Simba yalifungwa na Gerson Fraga mnamo dakika ya 14, Cloutous Chama (49), Louis Miquissone (51) na Mzamiru Yassin (88), huku bao la kufutia machozi la Yanga likipachikwa nyavuni na Feisal Salum ‘Fei Toto’ katika dakika ya 70. Kufuatia ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi Simba watakutana na Namungo FC ya Lind...

Desperados”: filamu mahususi kwa wanaoteswa na mapenzi

Image
Safari inaanza ya mabinti hao watatu kusafiri kwenda Mexico kumtafuta Jared na kuhakikisha haisomi barua ile. Picha|Mtandao. Inamuhusu mwanadada Wesley ambaye anaanza safari ya kumtafuta mwenzi wake wa maisha. Safari hiyo inaishia  katika majuto baada ya kutuma ujumbe wa kumtukana mpenzi wake bila kujua yaliyomsibu. Wesley na marafiki zake, wanafungasha virago kumtafuta Jared ili wahakikishe hasomi ujumbe huo. Dar es Salaam.  Ukisikia “majuto ni mjukuu” ndiyo hivi. Binti Wesley Darya (Nasim Pedrad) ambaye umri wake unazidi kwenda ana shauku ya kupata mtu wa kumuoa na hivyo anajikuta katika safari ya kutafuta mwenza wake wa maisha.  “Unaonekana kama binti mzuri sana lakini kwangu mimi wakati bado siyo sahihi,” ni maneno anayoambiwa na mmoja wa wadau anaokutana nao katika safari hiyo. Maneno hayo yanampelekea kuchanganyikiwa na kujikuta kwenye ajali ambayo baada ya kuamka, anakutana na sura ya Jared (Robbie Amell). “Ulikuwa wapi maisha yangu yote?”.Ni ...

Orodha ya vitu ambavyo vinaweza kukufanya kuonekana mzee kuliko umri wako

Image
Ushawahi kujistukia kwa nini unaonekana mzee sana kuliko umri wako? Au Ukijilinganisha na rafiki zako wenye umri kama wako wewe unaonekana Umri umeenda sana hata shikamoo haziishi? Basi Maadui Hawa hapa:- Sigara Kutokana na kiwango kikubwa cha sumu ziitwazo Free radicals(ROS) unazozipata kila unapo ingiza Pafu moja la sigara.  Sukari Kutokana na Kuzalisha Free radicals nyingi wakati wa mchakato wake Oxidation na huhatarisha mwili kuingia kwneye msongo wa sumu ziitwazo Reactive Oxygen species (ROS). Pia Sukari inakuhatarisha na Unene, Kisukari, shinikizo la damu, Pumu Vidonda vya tumbo, magonjwa ya homoni mabavyo vyote hivyo ni magonjwa yanayo chakaza mwili. Tafiti moja iliyofanywa na Dr solomon hapo Muhimbili ilionesha kwamba sampuli ya damu  kutoka kwa wagonjwa wenye kisukari ilipopimwa Kiwango cha Free radicals kwa kutumia Spectrophotometer  ilionesha kwamba wagonjwa waliokuwa na athari kubwa za kisukari walikuwa na kiwango kikubwa sana cha sumu hizo free radi...

VIDEO | Chege Ft. Mrisho Mpoto – Pekupeku

Image

Huamini ndoto zako? tazama filamu ya “The Story of Fire Saga”

Image
Ni filamu inayohusu marafiki wawili wenye ndoto za kushinda mashindano ya kimataifa. Changamoto ni kwamba, watashindaje huku hawajui kuimba? Kama una uwalakini na ndoto zako, huenda filamu hii ikakuamshia uthubutu. Dar es Salaam.  “Tangu tukiwa wadogo, tumekuwa na ndoto moja tu,” Sigrit Ericksdóttir (Rachel McAdams) anasema na Lars Erickssong (Will Ferrell) anajibu “Kushinda mashindano ya muziki ya Euro Vision.” Wawili hao ambao ni marafiki wa dhati tangu utotoni, wana ndoto ya kuwa wanamuziki mashuhuri wakiiwakilisha nchi ya Ice Land katika mashindano hayo makubwa katika bara la Ulaya kupitia bendi yao isiyofahamika iitwayo “Fire Saga”. Lakini wanawezaje kufikia ndoto zao iwapo Iceland ambayo wanatarajia kuiwakilisha, inawaona kama majokeri, wazee, wapitwa na wakati na wasio na swaga?  Tuache utani. Kwakweli, hata wewe huenda ungeomba kurudishiwa pesa yako endapo ungehudhuria baadhi ya matamasha yao. Wanawezaje kufikia ndoto zao iwapo Iceland ambayo wanatar...