CORONA KUBADILI TARATIBU ZA WANACHUO UDSM :

Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam imewataka wanafunzi wote wa UDSM watakapofungua chuo rasmi Jumatatu, Juni Mosi, kuhakikisha wanavaa barakoa (mask) muda wote wanapokuwa darasani na viunga vya chuo. Mbali na hilo, wanachuo hao pia wametakiwa kuhakikisha wanapowasili chuoni ni lazima watumie vitakasa. "Kila mwanafunzi utakapowasili chuoni utakutana na vitakasa mikono vya aina mbili vya kukanyaga kwa miguu na vya automatic ukiweka mikono inatoa sabuni na maji. Kila mwanafunzi atatakiwa kunawa mikono kila anapotoka sehemu moja kwenda nyingine,hususani anapoingia darasani na kutoka nje. Kumbuka vitakasa mikono vitawekwa maeneo yote ya kuingilia na kutoka madarasani na sehemu zote za mikusanyiko." ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya kwa wanafunzi. Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya kikao kilichoshirikisha uongozi wa serikali ya wanachuo na Wizara ya Elimu, jana Jumanne, Mei 26 kikao hicho kimeafiki pia kupunguza muda wa masomo kutoka wiki...