WIZI WA KAZI ZA WAANDISHI
MADA: *WIZI WA KAZI ZA WAANDISHI* Wapendwa, karibuni katika somo letu kuhusu wizi wa kazi za waandishi wa vitabu. Somo hili kwa kiasi ni gumu. Pengine, njia nzuri ya kuelewa somo hili ni kupitia kwanza somo la *Hakimiliki.* Ugumu wa soma hili unasababishwa na waandishi, wasomaji na jamii nzima kutofahamu kwa kina kuhusu hakimiliki za kazi za waandishi. Pili, ni kutokana na Hakimiliki zenyewe kuonekana kutofanya kazi kwa uhalisia katika mazingira ya Kiafrika. Nikuulize swali hapa, *Umeshasikia wezi wangapi waliokamatwa kwa wizi wa kazi za waandishi?* Aidha, tunapozungumzia wizi wa kazi za waandishi tufahamu kwamba ni neno pana na tata kidogo. Katika mazingira ya dini, utata unakuwa mkubwa zaidi. Kwa mfano, kuna vitabu ambavyo vimewekewa *Haki ya Kunakili* ambayo si funge. Kuna baadhi ya vitabu vinaweza kuandikwa kwamba kwa ajili ya Uinjilishaji basi kitabu hiki kinaweza kutumika bila ruhusa. Swali hapa linakuja kwamba *ikiwa kitabu ni cha kiroho, mipaka ya Uinjilishaji na is...