Binti fanya haya kumsaidia mpenzi wako kutimiza malengo yake
Unaweza kufanya hivyo kwa kumkumbusha kuweka akiba na hata kwa kumuonyesha vipaji vyake asivyoviona. Kwa kumsaidia yeye, itakupatia amani pale utakapoona amefanikiwa huku ukiwa na mchango kwenye mafanikio yake. Ni kweli unapenda vitu vizuri lakini siyo mbaya ukajinyima kwa muda. Dar es Salaam. Ni kwanini nimeamua kuandika makala hii? Ni swali nililojihoji hata mimi kabla sijaanza kuandika nilichoandika. Sababu kubwa ni hii "sasa mwanaume huna pesa mimi nakupeleka wapi?" kauli hiyo imetoka kwa mwanadada mmoja aliyekuwa akiwasimulia wenzake juu ya hali ya mpenzi wake. Hali hiyo ilinipatia mawazo ya mchango wa mwanamke katia kumsaidia mpenzi wake wanapokuwa kwenye mahusiano. Nimeongea na vijana wengi lakini jibu la Mike Goodwill limenivutia zaidi. Baada ya kumuuliza ni vipi anaweza kumridhisha mpenzi wake kiuchumi, alishika kichwa kana kwamba ameona Israeli anamfuata. "Acha tu kaka, kuna muda mwingine ninakuwa sina pesa alafu shemeji yako naye anakupig...