Silaha za ushindi zinazoweza kuwasaidia wanafunzi kidato cha sita 2019
Mwanafunzi ajiandae kiisaikolojia kwa kujenga fikra za kujiamini na kuhakikisha afya ya akili na mwili iko sawa kuukabili mtihani. Walimu wana wajibu wa kuwaandaa vema wanafunzi kwa kuwafundisha mbinu za kufaulu mtihani. Tathmini ya muda uliobaki kabla ya kufanya mtihani ifanyike ili kutoa kipaumbele kusoma notsi chache na masomo unayoyaelewa zaidi. Dar es Salaam. Kufeli sio jambo la kufurahisha kwa mtu yeyote iwe kimasomo au maisha. Hata kwa wanafunzi waliopo shuleni ambao wanategemea kutimiza ndoto zao kuelimika na kupata taaluma watakazozitumia kuendeleza maisha, kufeli ni moja ya masuala hawaombei wakumbane nayo. Lakini kufeli kunaweza kuepukwa ikiwa mwanafunzi amejiandaa vizuri kuukabili mtihani. Kufaulu mtihani kunategemea pia mbinu mbalimbali ambazo zikitumika vizuri zinaweza kumtoa mwanafunzi kimasomo. Wadau wa elimu wakiwemo wanasaikolojia na wahadhiri wa vyuo vikuu wameweka wazi mbinu wanazoweza kutumia watahiniwa wa kidato cha sita ambao wan...