Posts

Showing posts from December, 2018

JOHN BOCCO AWATISHA WAARABU

Image
Nahodha wa Simba, John Bocco, ameweka wazi licha ya kupangwa na timu mbili kutoka mataifa ya Uarabuni katika Ligi ya Mabingwa Afrika, wamejipanga kuweka rekodi kuhakikisha wanawafunga kila watakapokutana nao na kusonga mbele katika hatua hiyo. Bocco ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliosaidia kikosi hicho kutinga hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Afrika ambapo wamepangwa katika Kundi D. Kundi hilo lina timu za Al Ahly ya Misri, JS Saoura ya Algeria pamoja na AS Vita ya DR Congo huku mechi yao ya kwanza ya hatua hiyo wakitarajia kucheza Januari 11 mwakani. Bocco ameliambia Championi Jumatatu, kuwa wameona kundi ambalo wamepangwa na tayari wameanza kujiandaa kikamilifu kuhakikisha wanazifunga timu zote ambazo watacheza nazo katika Uwanja wa Taifa zikiwemo Al Ahly na JS Saoura. “Mashindano haya ni magumu na kundi tayari tumeliona, kwetu hili ni kundi zuri na tutapambana kwa ajili ya kusonga mbele katika kundi kwa kushika nafasi za juu. “Watu wamekuwa wakiona tukipoteza mara nyingi ...

TAKUKURU KUINGILIA KATI SAKATA LA RUSHWA YA NGONO VYUO VIKUU

Image
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) imeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuongeza jitihada zaidi za kuwajengea uwezo  wanafunzi na wahadhiri juu ya masuala ya rushwa hasa ya ngono kwa lengo la kupunguza au kumaliza kabisa tatizo hilo vyuoni. TSNP umesema kuwa rushwa ya ngono kwa sasa imeshamiri katika vyuo mbalimbali nchini hivyo inapaswa kukemea kwani inaharibu maisha ya wanafunzi ambao wanategemewa kuwa viongozi wa baadae. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu wa TSNP, Joseph Marekela alisema rushwa ya ngono vyuoni ni changamoto kubwa hasa kwa wanafunzi wa kike hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kuhakikisha kuwa  hakuna mtu anayepoteza haki yake ya msingi kwa kukataa kutoa rushwa hiyo ambayo si tu inapoteza utu wa mtu bali ni kinyume na haki za binadamu. Alisema mfumo wa upimaji uwezo uliyopo sasa umempa mamlaka makubwa mhadhiri ya kuamua hatma ya mwanafunzi kitaaluma jambo am...

KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA MBEYA CITY HIKI HAPA

Image
Kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Mbeya City leo 1. Ramadhani Kabwili 2. Paul Godfrey 3. Gadiel Michael 4. Abdalah Shaibu 5. Kelvin Yondani 6. Feisal Salum 7. Ibrahim Ajibu  8. Haruna Moshi Boban 9. Heritier Makambo 10. Amis Tambwe  11. Mrisho Ngassa Kikosi cha akiba 12. Klaus Kindoki 13. Juma Abdul 14. Cleofas Sospeter 15. Maka Edward 16. Deus Kaseke 17. Jaffary Mohamed 18. Pius Buswita

TOFAUTI YA SIMBA SC NA WAPINZANI WAKE KUNDI D LIGI YA MABINGWA

Image
KLABU ya Simba ya Tanzania imepangwa Kundi D pamoja na JS Saoura ya Algeria, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Al Ahly ya Misri katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika droo iliyopangwa usiku huu ukumbi wa Nile Ritz-Carlton mjini Cairo nchini Misri, Kundi A limezikutanisha timu za na Lobi Stars ya Nigeria, Wydad Casablanca ya Morocco, Asec Mimosas ya Ivory Coast na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Kundi B linaungwa na FC Platinums ya Zimbabwe, Horoya A.C ya Guinea, Esperance ya Tunisia na Orlando Pirates ya Afrika Kusini, wakati Kundi C limezikutanisha Ismailia FC ya Misri, CS Constantine ya Algeria, Club Africain ya Tunisia na TP Mazembe ya DRC. Simba imefuzu tena kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya miaka 15, kufuatia mara ya mwisho kufika hatua hiyo mwaka 2003 ikiitoa Zamalek ya Misri kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake. Na msimu huu wamefuzu kwa kuitoa Nkana FC ya Zambia kwa jumla ya mabao 4-3, waki...

REKODI YA SIMBA SC AFRIKA TANGU ENZI ZA MWALIMU

Image
Simba SC Na E. Mashele LIGI YA MABINGWA AFRIKA: MWAKA 1974: RAUNDI YA KWANZA: Linare (Lesotho) Vs Simba (Tanzania) l-3: l-2 RAUNDI YA PILI: Zambia Army(Zambia) Vs Simba (Tanzania) l-2:0-l ROBO FAINALI: Hearts Of Oak Vs Simba l-2:0-0 NUSU FAINALI: Simba Vs Mehallal 1-0:     0-1 (Mehalla ilishinda kwa penalti 3-0, ingawa kuna habari za kipa wa Simba, Athumani Mambosasa (sasa marehemu) kufanyiwa fujo, wakati wa upigwaji wa penalti. MWAKA 1977: RAUNDI YA KWANZA: Simba (Tanzania) Vs Highlanders (Swaziland) Highlanders ilijiotoa, Simba ikasonga mbele. RAUNDI YA PILI: Water Corp. (Nigeria) Vs Simba 0-0: l-0 MWAKA 1978: RAUNDI YA KWANZA: Simba (Tanzania) Vs Vautour (Gabon) 2-0: 0-1 RAUNDI YA PILI: Vita (Zaire) Vs Simba (Tanzania) 1-0: 1-0 MWAKA 1979: RAUNDI YA KWANZA: Simba Vs Mufulira Wanderers (Zambia) 0-4: 5-0 RAUNDI YA PILI: Simba Vs Racca Rovers (Nigeria) 0-0: 0-2 MWAKA 1980: RAUNDI YA KWANZA: ...