AINA ZA BAHARI YA USHAIRI WA KISWAHILI
Na E. MASHELE +255766605392 BAHARI ZA MASHAIRI Utenzi Utendi Ndiyo mashairi marefu katika shairi, huwa na kina aghalabu huzungumzia maswala ya kihistoria , mashujaa ,mapenzi na mengineyo. Huwa na kipande kimoja tu. Idadi ya mizani katika kila mshororo huwa kati ya mizani nne na kumi na mbili .kina cha mshororo wa mwisho aghalabu huwa kilele katika beti zote nacho huitwa kina bahari Mfano Nakuita hima janabi, Njoo katika ukumbi, Unipeyo rambi rambi, Ya hiki changu kili o , Kilio changu muhubiri, Nataka kukukatibu, Kiwe katika vitabu, Pamo na msaada o , Mifano ya utenzi Utenzi wa fumo liyongo utenzi wa uhuru wa Kenya Msuko Ni shairi lenye kibwagizo kifupi. Mfano i Mwajiona asumini, nanyi mmebahatika, Na waridi vitaruni,mwahisi hamna shaka, Pia viluwanmitini, nanyi mmeburudika, Mtahizika! Mf...