Viongozi wakubaliana Wahamiaji kuondolewa kwa dharura Libya
Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya na wa nchi za Umoja wa Afrika wanaokutana katika mkutano wa kilele nchini Ivory Coast wamekubaliana kuhusu mpango wa kuondoa nchini Libya wahamiaji wanaokabiliwa na mateso. Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara katika mkutano wa tano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya na wa nchi za Umoja wa Afrika kutoa wito wa hatua za dharura kuchukuliwa kukomesha biashara ya utumwa na mateso mengine dhidi ya wahamiaji yanayoendela Libya. Rais Ouattara amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya kila liwezekanalo kukomesha madhila wanayopitia wahamiaji. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyeongoza kikao cha dharura pembezoni mwa mkutano huo kujadili suala hilo la biashara ya utumwa Libya, amesema viongozi wa Libya, Ujerumani, Chad, Niger, Ufaransa pamoja na nchi nyingine nne na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika wameamua kuanzisha operesheni ya dharura kuwaondoa wahamiaji ha...