WATAFITI wa masuala ya afya na saikolojia wanasema tendo la ndoa ndicho tendo ambalo humpa furaha kubwa zaidi binadamu na endapo atafanya tendo hilo kwa amani, utulivu na furaha huku wakieleza kuwa kufanya mapenzi kuna faida nyingi.
 
Lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi unapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara tena kwa watu wanaoendekeza sana ngono katika maisha yao ya kila siku.
 
Kuna mtu hawezi kabisa kulala bila kufanya mapenzi, hawezi kupitisha siku bila kufanya ngono, wengine wanashindwa kuvumilia angalau siku mbili au tatu. Mtu ana mke, anataka kila siku afanye naye tendo la ndoa eti kwa sababu tu ni haki yake na hakuna wa kumzuia kufanya hivyo, sababu ametoa mahari.
 
Jambo hili linaweza kuwa jema kwa upande mmoja, lakini tafiti zinaonyesha kwamba miongoni mwa kesi za watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka, wengi wao wapo katika kundi la watu wapenda ngono kupita kiasi (wanaume na wanawake).
 
Wanawatolea mfano makahaba ambao wanafanya mara kwa mara, watu kama hawa wanatajwa kuwa hawana hisia za kimapenzi, hata kama zipo ni kiwango kidogo sana, wanafanya kwa sababu ni biashara jambo ambalo ni hatari kwa afya na saikolojia yake.
 
Licha ya tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema ukajifunza usiwe mtu wa kuendekeza tamaa za mwili, kiasi kwamba unalazimika kufanya mapenzi popote, wakati wowote hata kwenye nguzo ya umeme ama makaburini ili tu kuuridhisha mwili wako.
 
KUPOTEZA HAMU YA TENDO (Sexual Dysfunction)
Wapo watu ambao wana pupa za kufanya mapenzi, hawa hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa kufanya tendo la ndoa mara kwa mara.
 
Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu (katika mazingira ya kujumuika katika tendo).
 
Aidha, kukinai haraka staili za kimapenzi kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake, hivyo kupoteza mvuto naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
 
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa wakati gani, yeyote atakayemuona yeye analiswaga twende tu ili afurahie.
 
Kuna watu wanajiendekeza kufanya mapenzi mara kwa mara, hawa ni wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake, afya yake, background yake, hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa kutembea na watumishi wao wa ndani au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa, ndugu, watoto wa ndugu n.k kwa vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.
 
Dk. Rahul Hajare mtafiti wa Taasisi ya Indian Council of Medical Research anasema unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo au mkeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy/housegirl ili akuondolee kiu ya penzi.
 
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO
Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyopandikizwa moyoni mwako kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.
 
Iwapo ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo (libido).
 
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili. Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke.
 
Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha. Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.

KUPATA MAGONJWA
Igafamike kwamba watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa  wana tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo magonjwa ya ngono kama ukimwi na mengine.
 
Dr. Jen Gunter, anasema mwanamke hutengeneza milimita 1–4 za ute wa kurainisha uke kwa siku, hii husaidia wakati wa kufanya tendo la ndoa.
 
Mapenzi yasiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko na maumivu wakati wa tendo la ndoa na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.
 

Madhara mengine;

Maumivu wakati wa kukojoa (micturition)
Uchovu na usingizi kupita kiasi (drowsiness)
Misuli ku-paralaizi (dysarthria)
Kupoteza kumbukumbuku.
Kupata miwasho na mikwaruzo ya ngozi.
Kuongezeka/kupungua uzito
Kukosa usingizi (insomnia)
Matatizo ya misuli.
 

Ushauri wa bure, ni vema kwa wapenzi kupunguza kiwango cha kufanya mapenzi ili kuifanya miili iwe na uvumilivu unaoweza kumsaidia mtu kukaa kwa muda mrefu bila kumsaliti mpenzi wake hata kama atakuwa amesafiri mbali naye kimasomo, kikazi au kibiashara