Masshele Swahili
Tamathali za semi ninani?
Hii ni Msemo ambayo hutumiwa kutoka maana tofauti na maana za maneno yake.
Zifuatazo ni baadhi ya tamathali za semi 

i) Tashibiha, Huu ni ulinganishi wa vitu au halipo mbili tofauti kwa kutumia maneno kama vile, kama, mithili ya, Sawa na,  utadhani ni, Sawa na 

Kwa mfano, anaimba vizuri kama Ally kiba

ii) Sitiari, Huu ni ulinganishaji wa vitu au halipo mbili, na ulinganishaji huu huwa ni wa moja kwa moja 

Mfano Juma ni simba

iii) Mubalagha 
Huu ni uelezaji wa jambo  kwa kutia mno chumvi kuliko uhalisia.
Mfano 
Manyama ana tumbo kama gunia.

iv) Tashihisi, hii ni hali ya kuvipa vitu visivyo binadamu sifa za ubinadamu.
Mfano, Jua likasema siwezi kuendelea na safari

V) Taashira, Hii ni njian ya kutaja kitu Fulani  kwa lengo la kuwakilisha kitu au jambo jingingine.


vi) Taniaba, hii ni njian ya kutumia jina Fulani kwa namna ya ulinganisho ili kumaanisha kitu kingine. Ambavyo huwa na tabia Fulani linganifu.  Mfano kiongozi Huyu ni Idi amin wa kizazi hiki.

Tamathali nyingine ni kama

majazi, 
Tafsida
Dhihaka
na Ritifaa

www.masshele.blogspot.com