Mkurugenzi wa WHO atoa pole kifo cha Dk Ndungulile

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Ghebreyesus.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Ghebreyesus ametuma salamu za pole Tanzania kufuatia kifo cha mkurugenzi mteule wa shirika hilo kanda ya Afrika, ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile.

Kupitia ukurasa wake wa X, Tedros Gabreyesus amechapisha ujumbe akisema ” nimeshtushwa na kuhuzunishwa sana kusikia kuhusu kifo cha ghafla cha Dk. Faustine Ndugulile, Mkurugenzi mteule wa kanda ya Afrika wa WHO.
“Pole zangu za dhati kwa familia yake, marafiki zake, Bunge na watu wa Tanzania”.

Aliyekuwa Mkurugenzi mteule wa shirika hilo kanda ya Afrika, ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile.

Dkt Faustine Ndugulile alichaguliwa rasmi nafasi ya Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Agosti 27 mwaka huu, akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Dr Matshidiso Moeti.
Dkt Faustine Ndugulile amefariki hii leo Novemba 27, huko nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?