Epuka Mambo haya wakati wa ujauzito
Kama nilivyokwisha kueleza kwenye makala ya kwanza kuhusiana na Lishe kwa wajawazito, nilieleza kwamba Ongezeko la uzito kwa mjamzito ni kiashiria tosha kinachoonyesha kwamba ujauzito una afya njema.
Kuna mambo mengi yasiyopaswa kufanywa na mjamzito na leo tutadodosa baadhi kama ifuatavyo:
Mwanamke mjamzito hapaswi kunywa pombe. Unywaji wa pombe kwa mjamzito husababisha mjamzito kujifungua kabla ya muda, kuzaa watoto njiti (low birth weight babies), kuharibu mfumo wa ubongo au ufikiri wa mtoto na kuharibu mfumo wa viungo vya mwili vya mtoto.
Vinywaji vya Chai, kahawa, Energy na vyakula vya Chokoleti vina kilevi aina ya Caffeine, Utafiti wa kisayansi unasema kwamba kuzidisha sana kilevi cha Caffeine wakati wa ujauzito unaongeza uwezekano mkubwa wa kuharibu ujauzito (miscarriage). Kwa hiyo inatakiwa mjamzito apunguze matumizi ya vyakula hivi ili kunusuru ujauzito wake. Inatakiwa mjamzito anywe si zaidi ya kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa siku, pia kwa upande wa vinywaji vya Energy inatakiwa mjamzito anywe si zaidi ya mls 250 kwa siku.
Ingawaje kwa upande mwingine vyakula vya kupunguza uzito havina virutubisho muhimu vinavyotakiwa katika ukuaji na maendeleo ya mtoto aliyetumboni. Ongezeko la uzito kwa mjamzito ni ishara ya ujauzito wenye afya njema, kwa hiyo mjamzito asithubutu kupunguza uzito. Kusoma makala ya kwanza kuhusu “Lishe bora kwa wajawazito.”
Mjamzito haruhusiwi kutumia dawa zozote zile za matibabu pasipo kuruhusiwa na daktari, Kwa sababu dawa hizo huweza kuleta shida kwenye ujauzito ikiwa ni pamoja na kutoa ujauzito, shida ya kujifungua na madhara kwa mtoto aliyetumboni.
Mjamzito haruhusiwi kutumia madawa ya kulevya ya aina yoyote ile kama Unga (Cocaine, Heroine na nyinginezo) na bangi. Madawa hayo hupita kwa urahisi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na kuathiri ukuaji wa mtoto, vilevile dawa hizo husababisha mjamzito kujifungua kabla ya muda, kujifungua watoto njiti, mtoto kufia tumboni, watoto kufariki ghafra baada ya kuzaliwa kuanzia siku 0 hadi miezi 6 pia hadi kufikia miaka miwili.
Vilevile uvutaji wa sigara husababisha kuzaliwa watoto njiti, pia huharibu mfumo wa ukuaji wa mapafu ya mtoto na huongeza hatari ya kusababisha madhara ya mfumo wa upumuaji na kupata ugonjwa wa pumu (Asthma) kwa mtoto mara atakapozaliwa
Comments
Post a Comment