Mamba aliyeolewa na Meya

TUKIO la kustaajabisha limetokea huko San Pedro nchini Ufilipino ambapo Meya wa eneo hilo anayefahamika kwa jina la Victor Hugo ameoa na kufunga ndoa na mamba mwenye umri wa miaka 7.

 

Kabla ya tukio hilo, Alhamisi ya wiki iliyopita, mamba huyo alibatizwa na anatambulika kwa jina la Princess, siku iliyofuata Ijumaa ndipo ndoa ikafungwa ambapo bwana hurusi alimbusu mamba huyo mdomoni ingawa mamba alikuwa amefungwa mdomo asije kukinukisha katikati ya sherehe na kujeruhi watu.

Mamba akiwa kafungwa mdomo ili kuepusha asijeleta madhara

Watu walikula, kunywa na kusaza huku muziki ukipigwa na watu kuserebuka. Mama mtu mzima kwa jina la Elia ambaye alipewa kazi kuhakikisha harusi hiyo inaenda vizuri, amekaririwa akisema aliumiza sana kichwa kujua mamba huyo bibi harusi atavaa nini lakini hatimaye alipata gauni zuri na shela vilishoneshwa kwa ajili ya mamba huyo na kumpendeza vilivyo.

Mamba amebatizwa na kupewa jina la Princess

Wanakijiji hawakuishia kula na kucheza muziki tu, bali pia walipata nafasi ya kumbeba na kumshika bibi harusi huyo kwa jina la Princess na kuzunguka nae mitaani kwa furaha.

 

Pamoja na hayo, harusi hiyo ni ya kimila, mamba anaolewa ambapo watu wa kijiji husika wanaamini kuwa ni muunganiko wa nguvu za kibinadamu na nguvu za kimungu hivyo wanaamini wavuvi maeneo yao watavua samaki wengi, watavuna mazao mengi, kupata chakula kingi, mvua nyingi kunyesha na kila aina ya neema.