Wakenya wengi mtandaoni na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kwingineko wanaelezea mshtuko wao na wakizua mjadala kuhusu jina la kampuni mpya ya Naomi Osaka iliyozinduliwa.

Jina la kampuni ya vyombo vya habari lenye maana ''hana sehemu za siri'' kwa kiswahili ambayo Osaka amezindua kwa ushirikiano na bingwa mara nne wa NBA LeBron James - imezua taharuki na imekuwa ikivuma kwenye mtandao waTwitter.

Neno hilo kwa kawaida si la staha kutamkwa hadharani kwa maana ya Kiswahili.



Kituo cha runinga cha Kenya, Citizen, kimeandika kuhusu mada hiyo kikihoji kwa nini Wakenya wamekuwa wakijadili kwa kiasi kikubwa mtandaoni.

Kampuni ya utayarishaji imesema itakuwa ikitengeneza hadithi ambazo "ni maalum kitamaduni lakini za ulimwengu kwa watazamaji wote" na zinalenga "kushughulikia masuala muhimu ya jamii".


Chazo : BBC