FASILI ZA DHANA ZA FONOLOJIA
MOFOLOJIA

FONOLOJIA:
Fonolojia ni tawi la Isimu ambalo hushughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha. (Massamba na wenzake. (2001:183).

Fonolojia hushughulikia vipashio ambavyo hutumika katika lugha inayohusika. (Massamba na wenzake (2001:183).

Kwa fasili hizo tunaweza kusema kuwa Fonolojia ni tawi la Isimu ambalo hujishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha inayohusika.

MOFOLOJIA:
Mofolojia ni tawi la Isimu ambalo hujishughulisha na uchambuzi wa kanuni na mifumo inayohusu upangaji wa mofimu mbalimbali ili kuunda maneno katika lugha. Massamba na wenzake (2001:192).

Mofolojia ni kiwango muhimu cha lugha ambacho hujushughulisha na mpangilio wa vipande sauti vyenye maana. (Bakari, M. (1988:18).

Kwa fasili hizo tunaweza kusema kuwa Mofolojia ni tawi la Isimu linalojishughulisha na kanuni na mifumo ya upangaji wa mofimu katika kuunda maneno.

KUSIGANA KWA TAALUMA YA MOFOLOJIA NA FONOLOJIA:
Umbo la msingi la mofolojia hujulikana kama mofu ilihali umbo la msingi la fonolojia ni fonimu.  Mofu ni maumbo yanayowakilisha Mofimu na Fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachojihusisha na lugha mahsusi.  Mifano:
FONIMU ZA KISWAHILI NA KIPARE
MOFU ZA KISWAHILI
MOFU ZA KIPARE
-m, n, t, k, g, l, v
-i, e, a, o, u
Hizi ni baadhi ya fonimu katika lugha za kibantu kikiwemo Kiswahili na Kipare).
m – toto
wa – toto
m – ni mofu funge ya umoja
wa – ni mofu funge ya wingi
toto – ni mofu huru.

mwa-na
va-na
mwa – mofu funge ya umoja
va – mofu funge ya wingi

Matawi ya Mofolojia hutofautiana na matawi ya fonolojia.  Hii ni kutokana na kwamba matawi ya Mofolojia ni Mofolojia ya minyumbuliko ya maneno na Mofolojia ya uundaji wa maneno ilihali katika fonolojia kuna Fonolojia vipande na fonolojia arudhi. 

Matawi ya Mofolojia hushughulika zaidi na mbinu za uundaji wa maneno ilihali matawi ya fonolojia kuhusika na sauti za lugha mahsusi, namna ya utamkaji na vipamba sauti kwa ujumla.

Fonolojia hushughulikia muainisho wa vipashio vya lugha inayohusika, jinsi vipashio hivyo vinavyofuatana na kuathiriana ilihali mofolojia huhusika na maumbo ya maneno yenye maana kisarufi na jinsi yanavyoweza kuathiriana.  Mifano ifuatayo hudhihirisha muathiriano wa kimofolojia na kifonolojia. Rubanza I. Y. (1996:3-4).



KIFONOLOJIA
KIMOFOLOJIA
SAUTI
SILABI
MOFIMU
NENO
/p/ /t/ /a/ /g/  /i/  /o/
pa + ta + ga + gi + pi + go
pat – a
pig – o
pat – o
pit – a
pata
pigo
pato
pita

Katika mifano hiyo ni dhahiri kuwa sauti huungana ili kuunda silabi hususani muunganiko wa konsonanti na irabu katika kuunda silabi ilihali mofimu huungana ili kuunda neno.

KUSHABIHIANA KWA TAALUMA YA FONOLOJIA NA MOFOLOJIA:
Kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya fonolojia na uundaji wa maneno katika lugha yoyote iwayo.  Wanaendelea kusema kuwa, kwa upande wa mofolojia, maneno huundwa na mofimu na mofimu huundwa na sauti.  Aidha uundaji wa mofimu hufuata taratibu maalum za mfuatano wa sauti za lugha ihusikayo. Massamba na wenzake (2013:14).
Tuchunguze mifano ifuatayo katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kipare:
SAUTI
MOFIMU
MANENO
-          /p/ + /a/ + /t/ + /a/
-          /i/ + /m/ + /b/ + /a/
-          /k/ + /a/ + /t/ + /a/
-          /b/ +/i/+/g/+ /h/ + /a/
-          i + m + a
-          e + i + m + b + a
pat – a
imb – a
kat – a
bigh – a
im – a
e – imb – a
pata (kiswahili)
imba (kiswahili)
kata (kiswahili)
bigha (kipare – piga)
ima (kipare – lima)
eimba (kipare – anaimba).

Taaluma ya fonolojia na mofolojia zina uhusiano na zinategemeana. Rubanza Y.I. (1996:4). Anasema, uhusiano wa karibu wa folonojia na mofolojia unadhirika kutokana na mifano ifuatayo:-           Kushoto:                Kulia:
a)   Mu – ana        =          mwana
b)   Mu – anafunzi =        mwanafunzi
c)   Mu – alimu    =          mwalimu

Kipashio [mu-] katika jozi ya kushoto kinachodhihirisha umoja hujitokeza kama [mw-] katika jozi ya kulia, ambapo kanuni hiyo inazingatia taaluma ya kifonolojia na mofolojia.  Kanuni hiyo ni mu → mw - /- I ikimaanisha [mu-] inajitokeza kama [mw-] inapofuatwa na irabu ambapo katika mifumo hiyo ni irabu [-a-]

i → y / -  + a. Sheria hii inatuambia kuwa irabu juu inayotamkiwa mbele hubadilika na kuwa kiyeyusho kinachoendana nayo iwapo mbele yake kutakuwa na irabu chini inayotokea baada ya mpaka wa mofimu.  Massamba, (2012:19).
Mifano:
-          Kiswahili:        vi+ama = vyama
Vi+ake            = vyake
Vi+ao              = vyao
-          Kipare:            vi + avo           = vyavo (vya kwao).
Vi + enyu        = vyenyu (vya kwenu).

Uundaji wa mofimu za lugha ambao ni sehemu za mofolojia hufuata taratibu maalum za fonolojia ya lugha inayohusika.  Hii ndiyo maana tunasema kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya mofolojia na fonolojia.  Tuchunguze mfuatano wa sauti zifuatazo ambazo utaratibu wa fonolojia ya Kiswahili haukubali pamoja na lugha zingine za kibantu na kupelekea kuundwa kwa maandishi yasiyo na maana. Massamba na wenzake (2013:15)

SAUTI ZENYE MPANGILIO USIOKUBALIKA
UMBO LISILOKUBALIKA
MPANGILIO UNAOKUBALIKA
Sauti
Neno
/g/  /k/ /a/ /i/ /p/ /i/
/b/ /b/ /b/ / u/ /u/
/a/ /k/ /k/  /g/ /o/
gkaipi
bbbu
akkgo
/p/ /i/ /g/ /i/ /k/ /a/
/b/  /u/ /b/  /u/
/k/  /a/  /g/  /o/
pigika
bubu
kago


Vipashio vya kifonolojia ndivyo viundwavyo vipashio vya kimofolojia.  Hii ina maanda kuwa muunganiko wa sauti za lugha zikiwemo konsonanti, viyeyusho na Irabu hunda silabi na silabi huunga na kuunda maneno ambapo kimsingi uundaji wa sauti na silabi hufanyika kifonolojia ili kuunda mofimu kisha maneno ambayo ni mofolojia. (Rubanza Y. I. (1996:4).

MIFANO YA SAUTI
SILABI
MOFIMU
NENO (MAANA)
Kiswahili = /a//n//a//c//h//z//a/
Kiswahili= /w//a//m//e//f//u//a/
Kipare = /e//c//h//e//z//a/
Kipare = /v//a//f//u//a/
a+na+che+za
wa+me+fu+a
e+chez+a
va+fu+a
a-na-chez-a
wa-me-fu-a
e-chez-a
va-fu-a
Anacheza
Wamefua
Echeza (anacheza)
Vafua (wamefua)

Vilevile kwa upande wa Fonolojia silabi ni kipashio cha kiisimu ambacho hutamkwa kwa mara moja kama fungu la sauti linalojitegemea.  Katika mtazamo huihuo tunaweza kusema mofimu ni kipashio kidogo kabisa katika umbo la neno ambacho hakiwezi kuvunjwa na kugawanywa katika vipande vingine bila kupoteza uamilifu wake.  Massamba na wenzake, (2013:13). Tuchunguze mifano ifuatayo:
SILABI
IDADI
MOFIMU
IDADI
pi + ga + ni + sha
pa + ta
di + ri + sha
(silabi nne)
(silabi mbili)
(silabi tatu)
pi – ga – ni – sha 
pa – ta 
dirisha
(mofimu nne)
(mofimu mbili)
(mofimu moja)

Taaluma ya fonolojia inahusisha silabi huru na silabi funge jambo ambalo mofolojia nayo ina mofimu huru na mofimu funge. Silabi huru ni silabi zinazoishia na irabu ilihali silabi funge ni silabi zinazoishia na consonant.  Hali kadhalika mofimu huru ni mofimu zinazojitosheleza kimaana ilihali mofimu funge ni zile mofimu ambazo hutegemea mofimu zingine katika neno ili ziweze kujitosheleza kimaana.
Mifano:-
SILABI HURU                                            SILABI FUNGE:
Kiswahili:        - ba + ba = baba                      Kiingereza = father (baba)
                        - a + mu + a = amua                                  = fax (faksi)
Kipare             - va + va = vava (baba)                             = sector (sekta)
                        - a + mu + a = amua
Mofimu huru                                                 Mofimu funge
-          Fluri                                                     a + na + lim + a
-          Lea                                                      A = huwakilisha nafasi ya tatu umoja.
-          Rozina                                                 na = huwakilisha wakati.
lim = mzizi wa neno.
a = mofimu tamati.

Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kwamba taaluma ya fonolojia na Mofolojia ni matawi ya kiisimu ambayo hutegemeana kwa kiwango kikubwa katika kujenga lugha hususani muunganiko wa sauti katika kujenga silabi, muunganiko wa silabi kuunda mofimu na muunganiko wa mofimu katika kuunda maneno.


MAREJELEO:
Dr. Bakari, M. (1988). Analysis of Modern Swahili Texts and Language Skills. Nairobi: University of Nairobi.
Kyao, R. (1988). Kiswahili Sekondari. TUMI.
Massamba na wenzake, (2001). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam. TUKI.

Rubanza Y.I. (1996). Mofolojia ya Kiswahili. Dar es salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.