Mchezaji wa klabu ya Simba, Haruna Niyonzima, amesema hawezi akabadilika kiwango chake kama ilivyokuwa zamani.

Niyonzima ameeleza kuwa kiwango chake kinaweza kikaimarika zaidi kuliko hata alivyokuwa Yanga kutokana na hali yake inavyoendelea.

"Haruna wa sasa anaweza kuwa hata zaidi ya yule wa zamani, siwezi kusema kama kiwango changu kitashuka, mimi najiamini na naweza kuusoma mchezo haraka pale ninapokuwa Uwanjani" alisema wakati akihojiwa na kipindi cha michezo kupitia Radio One jana.

Aidha, Niyonzima amesema kuna watu wanadai kuwa kuhamia kwake Simba inawezekana ndiyo ikawa mwisho wa maisha yake ya soka, huku akieleza wasitegemee kuona hilo maana anajipanga kila kukicha.