Mama mwenye vvu anaweza kuzaa mtoto asiye na vvu endapo njia zote zinazoweza kumweka mtoto katika hatari ya kupata maambukizi zitazuiwa.


Ni vyema tukatambua kuwa mtoto anaweza kupata maambukizi toka kwa mama katika njia tatu muhimu.Njia hizo ni pamoja na mtoto anapokuwa tumboni,wakati wa kuzaliwa na wakati wa kunyonya maziwa ya mama.Hatari zaidi ni pale mama anapokuwa na idadi kubwa ya vvu katika damu na akawa anaugua mara kwa mara.Kwa jinsi hii usalama wa mtoto tumboni unakuwa ni mdogo na anaweza akapata maambukizi akiwa tumboni hasa pale mfuko wa uzazi unapokuwa dhaifu kiasi cha kuruhusu damu ya mama ichanganyike na ile ya mtoto.Maambukizi ya mama kwenda kwa kwa mtoto kwa njia hii ni kwa kiasi kidogo tu.Endapo kiasi cha vvu katika damu ya dawa ya kumkinga mtoto,hali ya mama itakuwa nzuri na uwezekano wa mtoto kupata maambukizi kwa njia hii huwa mdogo.

Wakati wa kuzaliwa mtoto anaweza kupata maambukizi toka kwa mama kama atapata michubuko mwilini mwake na mama akawa na michaniko katika njia ya uzazi.Asilimia kubwa ya watoto wanaozaliwa hupata maambukizi kwa njia hii.Kwa jinsi hii kama kiasi cha vvu ni kidogo katika damu ya mama mtoto anaweza kuwa salama kwani ngozi ya mtoto mara nyingi huwa imekingwa na aina Fulani ya mafuta yanayoweza kuzuia michubuko japo anaweza akapata michubuko  kidogo.

Wakati wa kunyonyesha mama anashauriwa kutompa mtoto chakula kingine hadi hapo atakapomuachisha kulingana na muda uliokubaliwa wa kunyonyesha.Hii ni kulinda ukuta wa ndani ya tumbo la chakula ambao ni laini na unalindwa na utando mwepesi usipate kuchubuliwa na chakula kigumu hivyo kupitisha vvu vinavyokuwepo katika maziwa ya mama mwenye maambukizi.

Huduma zinazopatikana kliniki kwa ajili wajawazito wenye vvu 

  • Elimu ya vvu na ukimwi
  • Huduma ya ushauri nasaha juu ya kuishi na maambukizi ya vvu,lishe na namna ya kuzuia maambukizi mapya
  • Elimu ya namna ya kumkinga mtoto asipate maambukizi ya vvu
  • Kuangalia maendeleo ya mtoto tumboni na baada ya kuzaliwa
  • Dawa maalumu za kumkinga mtoto dhidi ya vvu
  • Ushauri juu ya uzazi salama katika hali ya maambukizi ya vvu
  • Huduma ya upimaji wa vvu kwa watoto
  • Huduma za maambukizi ya vvu kama vile kupima cd4,na vipimo vingine vinavyohusiana
  • Mafunzo juu ya kukubaliana na changamoto mbalimbali za maisha
  • Kuanzishwa dawa za ARVs kama wametimiza vigezo

ARV zinavyomkinga mtoto na maambukizi

Jinsi dawa za kuzuia maambukizi kwa mtoto zinavyofanya kazi:

Kwa mama: zinapunguza idadi ya virusi katika damu hivyo kufanya afya ya mama iendelee kuimarika na kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto

Kwa mtoto: inakuwa ni kama kinga baada ya hatari ya kuambukizwa(PEP)kuteketeza kiasi Fulani cha maambukizi anayoweza kupata akiwa tumboni.

ARV na dawa za kumkinga mtoto na maambukizi
Dawa za ARV na zile za kumkinga mtoto kutopata VVU hazipaswi kuchanganya kwa sababu dawa zinazotumika kumkinga  mtoto dhidi ya VVU zimo ndani ya dawa za ARVs.

Tofauti kati ya ARVs na dawa za kumkinga mtoto na maambukizi
Tofauti ni kwamba mama mjamzito ambaye hajatimiza vigezo vya kuanza kutumia ARVs anapewa aina moja ya dawa za ARVs kumkinga mtoto wakati yule aliyetimiza vigezo anatumia dawa aina tatu. 

Kuendela na dawa za kumkinga mtoto baada ya ujauzito:
Mama anayetumia dawa za kumkinga mtoto kama hajatimiza vigezo vya kuanza dawa za ARVs ataacha kutumia dawa hiyo mara baada ya kujifungua. Endapo atakuwa ametimiza vigezo ataanza kutumia dawa za ARVs ataendelea kutumia dawa hizo kama kinga kwa mtoto na tiba kwake maisha yake yote. 

Dawa za kumkinga mtoto zinazuia maambukizi kwa mtoto kwa kiasi gani?
Kwa mama anayetumia dawa za kumkinga mtoto dhidi ya vvu uwezekano wa kuzaa mtoto asiye na maambukizi ya vvu ni asilimia hamsini kwani kuna vigezo vingi vinavyohitajika kuzingatiwa hadi mtoto azaliwe bila maambukizi ya vvu kama ilivyoelezwa hapo juu.Hata hivyo mpango wa kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto unaonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa hasa baada ya maambukizi kwa watoto wachanga kupungua miongoni mwa wamama wanaotumia mpango huo,wamama wengi wanaotumia dawa ya kumkinga mtoto au walioko kwenye dawa za ARV na ambao wanafuata ushauri wa kitaalamu wanajifungua watoto wasio na maambukizi ya vvu kuliko hapo awali.