Hali ya taharuki imezuka jioni hii katika eneo la Buguruni kwa mnyamani jijini Dar es Salaam baada ya bomba la Gesi linalopita maeneo hayo kuwaka moto na hivyo kuzua hofu miongoni mwa wananchi ambao ni wakazi wa eneo hilo.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika lakini pia hakuna mtu yeyote ambaye ameripotiwa kupoteza maisha ingawa baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara vimekumbwa na moto huo huku nyumba mbili zikiungua. Masshele Blog inaendelea kufuatilia chanzo cha moto huo.