Michael Emenalo linaweza kuwa jina jipya kwa mashabiki wa soka lakini sura ya Emenalo inaweza isiwe sura ngeni kwa mashabiki wa soka Epl haswa wanaoangalia michezo ya mabingwa watetezi Uingereza Chelsea.

Michael Emenalo alikuwa moja ya wakurugenzi wa masuala ya ufundi ndani ya klabu ya Chelsea ambaye pamoja na uwezo wake lakini anaijua vyema Chelsea kwani amekaa klabuni hapo kwa miaka kumi sasa.

Tangu Emenalo awe katika bodi ya ufundi ya Chelsea wamefanikiwa kushinda makombe ya Epl mara tatu, Europa mara moja na pia wamefanikiwa kombe moja la Champions League katika kipindi chake.

Lakini sasa baada ya miaka hiyo 10 hii leo Michael Emenalo ameamua kuachana na klabu ya Chelsea huku habari za ndani zikisema kwamba Michael Emenalo anaelekea kujiunga na klabu ya Monaco.

Habari ya Emenalo kuachana na Chelsea inazidi kukuza tetesi ya maelewano mabovu yanayotajwa kuwepo kati ya kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte na baadhi ya viongozi wa klabu ya Chelsea.

Habari nyingine toka darajani inasemekana kocha Antonio Conte amejikuta akiingia kwenye ugomvi mpya na beki wa klabu hiyo David Luiz jambo lililopelekea kumuweka nje katika mpambano zidi ya United.