MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI AJIRA MPYA 2023
Serikali imetengaza majina ya WALIOITWA KWENYE USAILI wa AJIRA mpya 2023 katika nafasi mbalimbali za AJIRA zilizotolewa mapema mwaka huu 2023.
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
JA.9/259/01/A/312
04/06/2023
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Kituo cha Kimataifa
cha Mikutano Arusha (AICC), Local Government Training Institute ( LGTI), Shirika la Elimu
Kibaha (KEC), National Institute of Transport (NIT), OFISI YA WAZIRI, Tanzania Library
Services Board ( TLSB), Tengeru Institute of Community Development (TICD), Taasisi ya
Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Shirika la Reli Tanzania
( TRC), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA), Water Institute, Bodi ya Filamu
Tanzania, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu
Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe
2023-05-12 hadi 2023-06-19 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi
watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia
maelekezo yafuatayo:-
i.
Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda
na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
ii.
Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa
(Mask) iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv.
Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho
cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
v.
Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
kutegemeana na sifa za Mwombaji.
vi.
Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of
results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips)
HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
vii.
Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
viii.
Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
ix.
Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
x.
Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi
zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xi.
Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa
kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
xii.
Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao
na kunakili namba ya usaili kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
xiii.
Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Jiji la Dodoma ni baridi hivyo
mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.
xiv.
Msailiwa haruhusiwi kuja na simu au kifaa chochote cha kielekroniki kwenye eneo
la usaili.
Download full advertisement in PDF bellow
Comments
Post a Comment