Editors Choice

3/recent/post-list

Watu 271 wanaoishi na maambukizi ya VVU watoroka huduma ya dawa Njombe mjiniJumla ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) 271 kati ya 16,594 halmashuri ya mji Njombe wametoroka kwenye huduma za dawa  kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuaminishwa na viongozi wa dini kuwa wamepona baada ya kufanyiwa maombi.

Imebainishwa kuwa kati ya hao wanaume 104 na wanawake 187.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi,mratibu wa kudhibiti ukimwi sekta zote (CHAC) halmashauri ya mji Njombe Daniel Mwasongwe alisema wanaendelea kuwatafuta ili waweze kurudi katika huduma.

"Jitihada tunazochukua katika kuwatafuta hawa watu 271 ni kuendelea kuwafuatilia kwa sababu katika kumbukumbu zetu huwa wanaacha namba za simu lakini vile vile kuna wahudumu ngazi za jamii ambao ndiyo wanawasimamia,lakini kuna changamoto ya baadhi yao kuandika taarifa za ambazo si sahihi katika vitabu vyetu vya kumbukumbu"alisema Mwasongwe.

Mwasongwe alifafanua kuwa ni vizuri viongozi wa dini waweze kupata elimu ya virusi va ukimwi na ukimwi ili waweze kuwasaidia waumini wao na sio kuwashawishi kuacha dawa.

"Baadhi ya madhehebu ya dini siyo yote tunapata kesi kuwa mtu ameacha dawa ukimfuatilia anakwambia mimi nimeombewa na mtumishi fulani kwa hiyo mimi nimepona.Naomba nitoe ushauri watu wasiache dawa hata kama ukiwa umeombewa lakini wasiache dawa,kuacha dawa ni hadi pale daktari au mtoa huduma atathibitisha sasa hana maambukizi ya virusi vya Ukimwi"alisema Mwasongwe.

Alisema kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu watu 12,423 walipima VVU kwa njia ya hiari,kushawishiwa na mtoa huduma kwa njia ya mkoba Kati yao 602 walikutwa na maambukizi.

Hata hivyo alisema kwa upande wa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,jumla ya watoto 197 walipima kipimo cha kwanza idadi ya watoto waliokutwa na maambukizi ya VVU ni mmoja sawa na asilimia 0.5.

Naye mgeni rasmi katika maadhisho hayo,makamu mwenyekiti wa halmashauri mji Njombe Filoteus Mligo alisema kuwa jitihada za mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi zinahitajika

Post a Comment

0 Comments