Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limevifungia vituo vya mitihani 24 sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote 17,935 vilivyofanya mtihani ambavyo vimethibitika kupanga na kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2022.


Vituo hivi vimefungiwa hadi Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshji wa mitihani, vituo hivi ni Kadama Primary (Chato), Rweikiza Primary (Bukoba), Kilimanjaro Primary (Arusha), Sahare Primary (Tanga), St.Anne Marie Primary (Ubungo, Dar es salaam) , 


Vituo vingine vilivyofungiwa ni Ukerewe Primary (Mwanza), Peaceland (Ukerewe), Karume Primary (Bukoba) , Al Hikma Primary (Dar es salaam) Kazoba Primary (Karagwe), Mugini Primary (Magu Mwanza), Busara (Magu, Mwanza), Jamia Primary (Bukoba) Winners Primary (Mwanza), Musabe Primary (Mwanza ), 


Vituo vingine vilivyofungiwa ni Elisabene Primary (Tunduma), High Challenge Primary (Arusha), Tumaini Primary (Sengerema Mwanza), Holele Primary (Mwanza) Must Lead Primary (Chalinze) Moregas Primary (Tarime) Leaders Primary (Rorya), Kivulini Primary ( Mwanza) , St Severin Primary (Biharamulo).