Editors Choice

3/recent/post-list

Gorbachev azikwa na mamia ya Warusi mjini Moscow



Warusi hii leo wametoa heshima zao kwa mwili wa kiongozi wa mwisho wa uliokuwa umoja wa Kisovieti Mikhail Gorbachev, katika mazishi yaliyofanyika mjini Moscow bila kuhudhuriwa na rais Vladimir Putin. 


Mamia ya waombolezaji, walipanga foleni kuuga mwili wa Gorbachev katika ukumbi wa kihistoria mjini Moscow. Gorbachev, alifariki dunia siku ya Jumanne akiwa na umri wa miaka 91, katika hospitali alipokuwa akipatiwa matibabu kwa maradhi ya muda mrefu. 


Akiwa madarakani kati ya mwaka 1985 na 1991, Gorbachev alitaka kubadilisha Umoja wa Kisovieti kwa mageuzi ya kidemokrasia, ambayo yalichangia kusambaratika kwake. Mwanasiasa huyo mashuhuri wa karne ya 20 alijizolea sifa katika nchi za magharibi kwa kumaliza vita baridi lakini akikosolewa na Warusi wengi kwa uchumi mbovu wa Moscow na anguko la himaya ya kisovieti.

Post a Comment

0 Comments