KUWA CRDB WAKALA

Benki ya CRDB kupitia mtandao wa CRDB Wakala imetoa fursa ya ajira kwa watanzania zaidi ya 20,000 ambao wamejitolea kutoa huduma za kibenki kwa niaba ya Benki ya CRDB. Mtandao wa CRDB Wakala unawawezesha watanzania wote walio wateja na wasio wateja wa kibenki kupata huduma zetu za kifedha kiurahisi popote walipo.

Faida za kuwa CRDB Wakala


Kufanya biashara na Taasisi kubwa inayoongoza kwa utoaji huduma za kifedha Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla
Kupata malipo mazuri kutokana na kutoa huduma kwa wateja wakubwa wa CRDB
Ongezeko la wigo la wateja katika biashara yako kwani kila meta wa CRDB atalazimika kutembelea biashara yako
Kuleta ufanisi katika biashara yako kwa usimamizi wa pesa kwani utakua unawatumikia wateja wa CRDB ambao hutoa pesa taslim mara kwa mara kwa hivyo kupunguza hatari ya kutokua na pesa taslim
Kuongeza uwezo kupitia mufunzo ya bure kutoka Benki ya CRDB katika masuala ya kijasiriamali, huduma za kibenki, na mbinu mbalimbali za kuzuia utakatishaji fedha na udanganyifu wa kifedha

Huduma zinazopatikana kwa CRDB Wakala


Kupata fursa hii kubwa ya Benki ya CRDB kama yakala na balozi wetu, unahitaji kufikia vigezo vifuatavyo;

Mtu lazima awe na biashara inayosimamiwa vizuri, inayoendeshwa kisheria na kuwa leseni halali ya biashara
Lazima biashara ifanyike katika jengo la kudumu lenye miundombinu sahihi kuweza kutoa huduma za kifedha na rasilimali watu kukidhi kiwango cha ufanisi wa utoaji huduma na usalama
Mtu/ biashara lazima iwe imeshafanya kazi kwa angalau miezi kumi na nane (18) kama inavyothibitishwa na leseni ya biashara iliyopita au cheti kingine cha usajili kabla ya tarehe ya maombi ya uwakala
Mtu/ bishara haitakiwi kua na rekodi mbovu ya ulipaji mikopo kutoka Benki yoyote au taasisi yoyote ya kifedha na inatakiwa kutunza hadhi hiyo kwa muda wote wa makubaliano ya uwakala
Mtu/ biashara haipaswi kufanya uwakala wa Benki kama biashara binafsi
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB au washirika wao hawaruhusiwi kufanya uwakala wa Benki kwa niaba ya benki
Lazima uwe na mtaji wa chini wa kufanya kazi wa Tsh milioni 2 ambao utatunzwa wakati wa makubaliano na ada ya maombi ya uwakala Tsh 236,000 isiyo na mrejesho mara tu wakala atakapoidhinishwa na makubaliano ya saini

Ikiwa unatimiza mahitaji ya hapo juu au umevutiwa na unahitaji maelezo zaidi, wasiliana nasi.


Anwani ya Posta:
S.L.P 268,
Dar es Salaam, Tanzania.

Tafadhali piga simu:
+255(22)2197700
+255(0)714197700
+255(0)755197700
+255(0)789197700

Barua pepe:
info@crdbbank.co.tz