1. Lugha ya Kiswahili inazo fonimu ngapi? Zioredheshe na kuzipa sifa zao za kifonetiki. Kwa kila fonimu toa mfano wa neno inamotokea.

2. Utatumia vigezo gani kuthibitisha kuwa hizo ulizoorodhesha ni fonimu za Kiswahili?

3. Angalia data zifuatazo za lugha ya Kishambala

a) ganda (ganda)

h) ughoe (kamba)

b) ginta (chovya)

i) ghula (nunua)

c) gonda (andika)

j) ghotoka (rudi)

d) guha (mkuki)

k) mghanga (mganga)

e) ogoha (ogopa)

l) ghenda (tembea)

f) aga (aga)

m) ighuta (shiba)

Sauti [g] na [g] (gh) zina hadhi gani katika lugha hii? Thibitisha jibu lako.

4. Ikiwa maneno yafuatayo ya Kiswahili yangekopwa katika lugha ambayo haina sauti zilizoonyeshwa kando, yangetamkwaje? Kwa nini?

a) harufu

[r]

e) shamba

[Å¡]

b) Khamis

[kh]

f) zamani

[z]

c) dhahabu

[d]

g) theluthi

[q]



h) ghadhabu

[g], [d]

5. a) Onyesha tofauti zilizopo kati ya fonimu irabu za Kiingereza na zile za Kiswahili.

b) Ni fonimu irabu zipi za Kiingereza zingeweza kumpa shida sana mzungumzaji wa Kiswahili? Kwa sababu gani?

6. a) Nukuu maneno yafuatayo ya Kiingereza kama ambavyo ungeyatamka:

i) bat
ii) bud
iii) cat
iv) cart
v) favour
vi) favourable
vii) equate
viii) equality
ix) success
x) successive
xi) principle
xii) principal

b) Angalia matamshi ya maneno hayo katika kamusi ya Kiingereza, na ulinganishe na matamshi yako uliyonukuu. Kuna tofauti zozote? Katika maneno gani?

c) Unazielezaje tofauti hizo, kama zipo?

7. Angalia matamshi ya maneno yafuatayo ya mzungumzaji mmoja wa Kiswahili:

i) khaa
ii) khamba
iii) khisu
iv) khelele
v) khesi
vi) kule
vii) koti
viii) kula
ix) mkaa
x) shikilia
xi) mikebe
xii) shuka

a) Sauti [kh] na [k] zina hadhi gani katika data hizi?

b) Unafikiri ni sauti nyingine zipi za Kiswahili cha mzungumzaji huyu zina hadhi sawa na hizo za hapo juu? Jaribu kutoa mifano.

8. Angalia sauti [e] na [e] za lugha ya Kihispania:

a) pesa

(uzito)

f) peska

(kuvua)

b) vena

(msuli)

g) venga

(njoo)

c) pera

(tunda)

h) perla

(tunu)

d) pape

(alimeza)

i) papel

(karatasi)

e) come

(anakula)

k) comen

(wanakula)

Je, sauti [e] na [e] ni alofoni za fonimu moja au zinawakilisha fonimu mbili tofauti? Kama ni alofoni za fonimu moja, bainisha mazingira ya kifonetiki ya kila irabu.

9. Angalia sauti [t], [c], na [ts] za lugha ya Kijapani:

(1) tatami

(mkeka)

(11)

tsukue

(dawati)

(2) tegami

(barua)

(12)

ato

(baadaye)

(3) cici

(baba)

(13)

deguci

(toka)

(4) sita

(chini)

(14)

tsutsumu

(funga)

(5) matsu

(ngoja)

(15)

kata

(mtu)

(6) natsu

(kiangazi)

(16)

tatemono

(jengo)

(7) cizu

(ramani)

(17)

te

(kiganja)

(8) koto

(hoja)

(18)

uci

(nyumba)

(9) tomodaci

(rafiki)

(19)

otoko

(a kiume)

(10) totemo

(sana)

(20)

tetsudau

(msaada)

Sauti [t], [c], na [ts] ni alofoni za fonimu moja:

a) Onyesha mgawo wao
b) Nukuu kifonimu data uliyopewa.