Kuku amenivunja mguu ndotoni"

 


Msanii wa muda mrefu hapa nchini wa Tanzania, Hussein Jumbe amefunguka kusema madhara aliyopata hadi kuvunjika mguu yametokana akiwa ndotoni ambapo ameota alikuwa anapigana na kuku.



Msanii wa muziki wa Dansi Hussein Jumbe


Akifunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, Hussen Jumbe amesema ni ngumu mtu kuamini tukio hilo ila ukweli ndiyo na mtu pekee aliyetokea kumsaidia alikuwa ni mke wake ambaye alimshutua kutoka usingizini.


"Nimevunjika mguu nikiwa ndotoni ambapo niliota napigana na kuku, mimi nilikuwa naendesha baiskeli sasa kuna mtoto alikuwa ameshika manati ambayo aliipiga baiskeli yangu, nikamfuata wakati nagombana naye ghafla akageuka kuku, mimi nikawa nampiga ili asiniparue kumbe nilikuwa napiga kitu kizito kwenye mguu nikiwa kitandani ndipo mke wangu akanisaidia" ameeleza Hussein Jumbe


Aidha Hussein Jumbe amesema alijaribu kwenda kwa watafsiri wa ndoto ambao walimwambia kuwa tukio hilo linahusisha masuala ya kishirikina.

Credit EATV

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?