Imeelezwa kuwa kiungo wa zamani wa Simba ambaye alikuwa anaichezea timu ya African Lyon, Haruna Moshi 'Boban' amejiunga na timu ya Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili.

Habari za ndani ya Yanga zimeeleza kuwa kiungo huyo ambaye alikuwa ni msaada ndani ya African Lyon amejiunga na Yanga baada ya viongozi kuvutiwa na uwezo wake.

"Zahera alivutiwa na uwezo wake hasa mara baada ya kumuona akicheza kwenye mechi za ligi kuu na pia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga ulizidi kuwashawishi viongozi," kilieleza chanzo.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Hussen Nyika amesema kuwa suala la usajili bado lipo mikononi mwa kocha hivyo kama kuna mchezaji atapendekeza atasajiliwa ili aongeze nguvu ndani ya kikosi.

"Suala la usajili kwetu lipo chini ya Kocha Mkuu, hivyo mipango ikikamilika kila kitu kitakuwa hadharani mashabiki wasiwe na wasiwasi," alisema