Editors Choice

3/recent/post-list

MAJUTO: “MIMI NI MZIMA, NIKIFA MNIZIKE KWA WINGI”, AMTAJA KANUMBA



  • BAADA ya kusambaa kwa taarifa katika kimtandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Muigizaji Mkongwe nchini, Mzee Amri Majuto, amezungumza na kuwahakikishia Watanzania kwamba yeye ni mzima wa afya na anaendelea na matibabu yake baada ya kurejea kutoka India.

    Akizungumza kutoka nyumbani kwake, mzee Majuto amewataka Watanzaniawote waendelee kumuoombea ili afya yake irejee huku akiipongeza Serikali kwa kumsaidia kwenda kutibiwa India.

    “Niwaambie Watanzaania kwamba wasishtuke mimi sijafa, ni mzima jamani, kama Mwenyezi Munguatanichukua, basi mje mnizike kwa wingi, mniombee niende mahali pazuri. Mlimpenda sana rafiki yenu Kanumbalakini Mungu akampenda zaidi, kwa hiyo Mwenyezi Mungu ndio anatupenda zaidi,” amesema Mzee Majuto.

    Taarifa za kuzushiwa kifo kwa mkongwe huyo zimeanza kusambaa mapema leo Juni 26, 2018 asubuhi ambapo mwanaye, Hamza Majutioalikanusha taarifa hizo na kusema mzee wake huyo ni mzima wa afya ana anaendelea na matibabu nyumbani kwake.

    Post a Comment

    0 Comments