Kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery.
Unai Emery wa Sevila amethibitishwa kuwa Kocha mpya wa Arsenal baada ya tetesi zilizoenea kwa zaidi ya saa 24 zilizopita.Akizungumza baada ya kutambulishwa Unai alisema; “Nimefurahi sana kujiunga na klabu kubwa kwenye soka. Arsenal inajulikana na inapendwa sana duniani kutokana na staili yake ya mchezo.


“Inathamini wachezaji vijana, ina uwanja mzuri na hata inavyojiendesha imekuwa ikivutia wadau wengi sana ulimwenguni, ninajiskia raha sana kujiunga na jumuiya hii,”alisema.
“Ninaanza historia mpya ndani ya Arsenal.”

Hata hivyo, upepo ulibadilika juzi na sasa kocha huyo ambaye ameipa PSG makombe yote ya ndani msimu uliopita lakini mwishoni mwa msimu akatimuliwa.