Habari za muda huu mpenzi msomaji wa tovuti hii , Huunaomba nikulike siku ya leo ilweze kujifunza kwa pamoja magonjwa ambayo watu wengi sana huugua kutokana na kujamiana.

Kwanza kabisa kabla sijaorodhesha magonjwa hayo naomba nikuleze ni nini maana ya magonjwa ya ngono?

Magonjwa ya ngono ni magonjwa ambayo huenezwa wakati wa tendo la kujamiana. Kwa ufupi ni magonjwa ambayo uenezwaji wake hutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia ya tendo la ngono. Lakini pia naomba utambue ngono ya aina yeyote ile huweza kueneza magonjwa ya ngono au kwa kimombo huitwa ( sexual Transimution diseases).

Lakini ikumbukwe ya kwamba magonjwa yeyote ambayo huenezwa kwa njia hii ya ngono huwa hayana dalili, bali pindi mtu anapohisi ya kwamba huenda ukawa umeyakwaa magonjwa haya ni vyema akaenda kituo cha afya kwa ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa hayo.

Lakini yote tisa, kumi ni kwamba mtu ambaye amepatwa na magonjaa haya ya ngono yupo hatarini zaidi kupata maambukizi ya Virusi Vya ukimwi.

Yafutayo ni aina ya magonjwa ya ngono ambayo watu huugua mara kwa mara.
  1. Kaswende.
  2. Virusi vya UKIMWI.
  3. Human Papilloma Virus.
  4. Klamidia.
  5. Virusi vya Ini- hepatitis B.
  6. Genital Herpes.
  7. Kisonono.
  8. Trichomonas.
Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada, tunakusihi uendelee kutembelea Masshele blog karibu tena