Tatizo hili limekua linawakumba watoto wengi,tafiti zinaonesha takribani asilimia 70% ya watoto wanaozaliwa duniani hupatwa na hali hii.Jamii mablimbali wamekuwa wakilihusisha na imani za kishirikina.

Mtoto mchanga anaweza kuzaliwa matiti yamevimba au kuzaliwa yuko kawaida ndani ya siku mbili akuvimba matiti,mara nyingi matiti ya mtoto mwenye tatizo hili yanauma ukiyagusa mtoto analia,pia matiti ukiyakamua yanatoa majimaji na saa nyingine hutoa maziwa.
Wataalamu wanasema maziwa haya yanayotoka yanakuwa sawa na maziwa ya mama yanakuwa na virutubisho sawa na maziwa ya mama.

TATIZO HILI LINASABABISHWA NA NINI?
wakati wa kukaribia kujifungua ndani ya mwili wa mama Kiwango cha hormone ya Estrogen hushuka ili kuruhusus mwili wa mama kuanza kuzalisha hormone ya prolactin.Hormone ya estrogen Huzalishwa kipindi cha ujauzito ili kuimarisha mji wa mimba kipindi chote cha ujauzito,na hormone ya prolactin husaidia kutengenezwa kwa maziwa ya mama.
Wakati hayo yakitokea kwenye mwili wa mama pia kushuka kwa hormone ya Estrogen kwa mama kunapelekea mwili wa mtoto pia kutengeneza hormone ya Prolactin(hormone ya maziwa),mwili wa mtoto nao unaanza kutengeneza maziwa lakini kwa kuwa tezi za maziwa na mirija ya maziwa haijatengenezwa kikamilifu kwa mtoto inapelekea maziwa au majimaji kushindwa kutoka na kupelekea matiti kuvimba.

Saa nyingine hali hii hupelekea wadudu kuingia na kusababisha tatizo la kutunga usaa kwenye matiti hali inayojulikana kama Mastitis.

MATIBABU
Tatizo hili halihitaji dawa,baada ya muda tatizo hili huisha lenyewe.Mtoto atapewa dawa Ant biotics pale atapokuwa na dalili za matiti yake kutunga usaa.
Usimkamue mtoto.wapo baadhi huwakamua watoto wakidhani wanawasaidia lakini kukamua ndio inazidsha tatizo kwani unafanya matiti ya mtoto kuzalisha zaidi maziwa au majimaji na kumwongezea hatari ya kutunga usaa.