Bilionea wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’.
HAKIKA vita ya wakubwa watoto wanatakiwa kukaa mbali, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya bilionea wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, kudaiwa kutaka kupeleka maumivu kwa mara nyingine tena makao makuu ya Klabu ya Yanga.
Hivi karibuni, Mo aliwatibua Yanga baada ya kuikwamisha klabu hiyo kumuongezea mkataba mwingine Mnyarwanda Haruna Niyonzima na kumshawishi kwa mamilioni ya fedha kujiunga na Simba. Inadaiwa Mo amemwaga dola 50,000, zaidi ya Sh milioni 110 ili kumnasa Niyonzima.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi.
Inadaiwa kuwa mbinu hiyo pia anataka kuitumia tena ili kuipora Yanga kiungo wake mshambuliaji, Juma Mahadhi. Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Masshele blog imezipata zimedai kuwa, hivi sasa uongozi wa Simba upo katika mazungumzo na Mahadhi ukimshawishi aweze kujiunga na timu hiyo licha ya kuwa bado na mkataba wa mwaka moja na Yanga.
“Bado tunaendelea na zoezi letu la usajili kama kawaida lakini kwa wachezaji wa ndani tumebakiza nafasi mbili ambapo moja tunataka kumsajili Erasto Nyoni wa Azam na tupo katika
mazungumzo naye. “Lakini pia tupo katika mazungumzo na Juma Mahadhi wa Yanga kwani tunamtaka mchezaji huyo na mambo yakikaa sawa, tutamsajili muda wowote kwani bosi wetu ametuambia tumuambie avunje mkataba wake,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Alivyoulizwa kuhusiana na suala hilo, Mahadhi alisema: “Sina chochote cha kusema kuhusiana na hilo ila mimi bado ni mchezaji wa Yanga.” Lakini alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ili aweze kuzungumzia usajili huo, hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita tu bila ya kupokelewa.

KUJIUNGA NA PARMACH TZ NA KUPAKUA PARMACH APK 

BOFYA >>>HAPA>>> kisha jaza taarifa zako udeposit kupokea bonasi