Ukoo Ni muunganiko wa kimbari ambao huunganisha familia zilizo na chanzo kimoja (Mababu) ukoo huweza kukua na kupelekea kugawanyika kwa vitongoji kadhaa. Vilevile ukoo huweza kugawanyika kwa sababu za kigeografia. Katika makala hii tutazungumzia ukoo wa Mashelle ambao unaasili ya Mkuu, Shimbi. 

HISTORIA YA SHIMBI

Uruka wa Shimbi (nchi ya Shimbi)

Ukoo wa Maria kawishe (Kavishe) Shimbi ndio chanzo hasa Cha Mashelle. Ukoo huu wa Maria kawishe ukianza Shimbi Karne nyingi zimepita na mwanzilishi wa ukoo huu aliitwa M'mamba aliyetokea mamba kwa kirie na wakati akitafuta makazi mapya ardhi yenye rutuba ndipo alipoweka maskani yake katika uruka wa Shimbi (nchi ya Shimbi) na hapo ndipo ukoo wa Maria kawishe ulipoanzia. 

Kwa mujibu wa sensa ya wanaukoo mwaka 1993 hivi ndivyo vizazi vya wanaukoo

M'mamba akamza Kitimbiri, Kitimbiri akamzaa Ileti na Makaviha

A. Ileti akamzaa Mhambo, Latemba, Msheve  na Kisinga.

Mahambo akamzaa, Rimbisha, Kiorumu na Kituunga. 

Latemba akamzaa Kivese na Sangio. 

Msheve akamzaa Mlesani , na Kasimiri

Kisinga akamzaa Mboloso.

B: Makaviha akamzaa Mashaare, katika  uzao wa Mashaare  akawazaa Lamasawe, Mashelle na Mkave Pia Mshakai , Masaule, mwashile & Kyauka , Mshau & Mriaumbe.

Sasa tutahamia Kizazi Cha Mashelle ambalo ndio lengo hasa la  makala hii

N.B. vizazi vitakavyowekewa mabano wamezaliwa kwa mama mmoja. Tutakumbuka kuwa Mashelle alikuwa na wanawake wengi (mitara) 

1. Mashelle akamzaa (Leina & Stambuli ) , (Karufu &Stamesa) , Marikoso  na Kastabu

Marikoso akamzaa Ameli , Ameli akawazaa Juma, Revokati, (policarp & Francis) Juma akamzaa Narsis, Revokati akamzaa Rustus

2: Mashelle akawazaa Tena Rabdiel na Daudi.

Rabdiel akamzaa Michael na (Felisian, baltazari, na Reginald) Michael akamzaa Edgar

Daudi Akawazaa Joseph , Gasper, na (Leonard , Rogasian, Adelin, Just, Joachim, na Evodi) 

Joseph Akawazaa (Florian, Beda, Priscus)  Gasper Akawazaa (Edward na Bruno)

3:  Mashelle Akawazaa tena

Salia , Baiseli, Samuel na Mtafanye(selasin).

Salia akamzaa (Joseph , Sabas, Policarp na silvest) 

Baisel akamzaa Machakos Na (Gasper Joseph na Nolascos) 

Samuel akamzaa (Dominic &Severing) 

Mtafanye akamzaa Mark

Machakos Akamzaa Tablei

Mark akamzaa (Alexander Living & Cosmas)

4: Mashelle Akawazaa Tena 

Sabini, Fulani, na Faradi

Sabini Akawazaa Didas, Roman na Saturnine

Didasi akamzaa Evodi, 

Romani akamzaa (Felician & Frederick

Fulani Akawazaa (Simon , Elia & Victus)

Faradi akawazaa Joseph & Gasper


5: Mashelle Akawazaa Tena 

Leseri, Tilisho, Rajabu, Sausiku

Leseri kamzaa Aloise

Tilisho Akawazaa(Peter &John 

Rajabu Akawazaa (Pauli, Damas, Alexander na Peter) 

6. Mashelle Akawazaa Tena 

Abeid na Afnail

Abeid Akawazaa

Armogast, Tarimo na Antipas

Afnail Akawazaa, Bonifas, Adelin, na Peter

Armogast Akawazaa Oscar , Emmanuel, na Osmund 

Tarimo akamzaa Vinus

Bonifas akamzaa Beatuce, 

Adelin akamzaa Donacian na Fidelis

Peter Akawazaa(John , Thad3i, Fulgence, Frederk

7: Mashelle Akawazaa Tena 

Hamisi na Kashili

Hamisi akamzaa Roki, Akwilin, Michael, iddi

Roki akamzaa Venance, Makarius, Liberati, Luka

Akwilin akamzaa Edward na Josephat

Michael akamzaa Christopher

Iddi akamzaa Abas na Hemed

Kashili akamzaa, (Michael Ferdinand, Clemence , Gabriel na Aristark)

8: Mashelle Akawazaa Tena

Ndesaika , Kashomba (cosma)  na Kisawani

Ndesaika Akawazaa Faustin na prosper

Kashomba Akawazaa Roman na Edward 

Kisawani Akawazaa  wilbard , Adams, Orest, Paul, Thomas na Gasper (baba yangu) 

Faustin Akawazaa Morgan , Innocent, Daudi, Lasco, na novatus.

Roman Akawazaa Cosmas, Jamhuri, na Alois, 


9. Mashelle akamzaa Tena Leina

Leina Akawazaa Masumbuka, William, Francis, na afrika 

Masumbuko Akawazaa Prosper na chrispn 

William Akawazaa Joseph , Policarp, Ludovic nestory na Mathias


Francis akamzaa John , Afrika akamzaa Didas na John

John akamzaa Alfred , Didas akamzaa Joseph 


Leina Akawazaa tena

 Stephen na (Joseph, Roman, Damas, Adolf, na inyasi 

Stambuli Akawazaa Shauri, baltazari, na Gasper

Baltazari Akawazaa (bonifasi, Beati, Daniel na Bazili

Karufu akamzaa Satoti na Fasili

Satoti akamzaa  Pauso Gabriel na Policarp 

Pauso akamzaa Mosoi, Joseph, Paul, Ludovic na Colman

Gabriel akamzaa living na Vicente

Fasil akamzaa Yohan Na Dismas

Yohani akamzaa Andrea na Maroni

Dismas akzaa Karoli

Karufu akamzaa pia Thadei na Francis

Thadei akamzaa Justi, Wilhelm , Ulirk, na Innocent.

Francis akamzaa Joseph , Romani, Avelin na Modest.

STAMEZA

Akawazaa  Kalist , Winston Damas, na Michael 

Kalist akamzaa Hermeti, Perfect, na Regoberto

Winston akamzaa Deograsias na Valentin 

Damas akamzaa, Revokati, Christopher, Deonis, Victoria, na Frimin, 

Michael akamzaa, Eliuter na Isdor

STAMEZA Akawazaa Tena 

Shilven , Eugen, Salvator, Policarp

shilven akamzaa Ladislaus, na Edmund

Eugen akamzaa, Gido na Novati,

Salvator akamzaa Abauku, nocholaus na Geming, 

Policarp akamzaa , Gasper, Silvest Thadei na Priscus

KIZAZI KILICHOHAMIA SHIMBI TOLA USERINA KUKAA KWA MANGI MASHELLENA KUSHIRIKI MAMBO YOTE YA UKOO KATIKA KITONGOJI CHA KARUFU

Kimoruru akamzaa Issa, isaa akawazaa Wilbard na Pascal

Wilbad  Akawazaa Ulirk , Leonard, Edward na Francis, Pascal akamzaa Silvest

Vipi vizazi vingine vya Ndugu wa Mashelle ambavyo havitaoredheshwa hapa.

Napenda kuomba Radhi kwa mababu niliotaja majina Yao hapa. (Ngsameheni hai Kavishe)

HISTORIA YA SHIMBI  

UTAWALA WA MANGI MASHELLE SHIMBI

Kunako Karne ya 16 na 17 katika nchi ya wachagga kulikuwa na utawala wake na viongozi wakuu waliitwa Mangi. Katika nchi ya Shimbi nako walikuwa na Mangi wake. Historia ya umangi Shimbi ilianza kwa mzee Makaviha mwana wa pili wa mzee Kitimbiri, na mjukuu wa mzee, M'mamba. Ilikuwa Ni deaturi kurithishana umangi hivyo mzee Makaviha alimrithisha umangi ndugu yake Latemba. Latemba akamwachia umangi mzee Mashaare, Mashaare avivyozeeka akamrithisha umangi mwanae mkubwa Lamasawe,  baadaye Lamasawe akamrithisha umangi kwa mwanae mkubwa Matolo, muda mfupi baadaye Lamasawe aliuliwa  kwa viata vya kuvizia "kisooki" ambapo wakati huo Mangi Matolo alikuwa katika nchi ya Usseri karibu na Kenya baada ya kupata habari za kuuliwa kwa baba yake alifuka Shimbi Haraka  kwa kuwa wauwaji walikuwa bado hawajaondoka wakamuua Mangi Matolo  Ni Nia ovu ya kuuamgamiza utawala wa shimbi. Baada ya matukio hayo wananchi wa shimbi wakikubaliana wamwito ndugu wa Lamasawe , mzee Mashelle aliyekuwa uhamishoni huko uruka wa masharti ili aje awe Mangi Shimbi. Mashelle alikubali na akaiongoza Shimbi kwa mafanikio makubwa.  Baada ya mzee Mashelle kuzeeka akamchagua mwanae mkubwa Mzee Leina kuwa Mangi wa Shimbi. 

Mzee Leina Aondolewa Umangi , Mzee Mashelle arudia Umangi Shimbi.

Ilivyokuwa, Mangi Leina alikuwa na makarani wawili ambao walikuwa Ni Ali masharo na na victory kishindwa ambao walimwibia Mangi Leina shilingi 30  wakala njama na Mangi Selengia wa mkuu. Hata Mangi Leina alivyoenda kukopa fedha misheni mkuu , Mangi Selengia wa uruka wa mkuu alimshawishi padri asimkopeshe Mangi Leina TSH 30. siku ya kukusanya mapato kwa dc wa Moshi fedha ya Mangi Leina ilikuwa pungufu na hivyo kufukuzwa Umangi , Mangi wa uruka wa Usseri Mangi Sengua alipendekeza baba yake Leina mzee Mashelle arudishwe kuwa Mangi wa Shimbi mpaka alipofariki 1993. 

Wasaidizi wa Mangi MASHELLE

1. Mashami, mzee Tamira ibara

2. Masho, mzee mwasu, na baadaye marema Moshivira

3. Issia mzee kitara matere

4. Kitirima mzee Manguo mashombo

5. Uua. Mzee ngumia Teng'ute 

Shimbi Yatawaliwa na Mangi Selengia wa Mkuu: Baada ya Mangi Mashelle kufariki 25.12.1923 , mwanaye aliyekuwa Mangi, Leina alienda Moshi kudai umangi lakini alikataliwa na hivyo Mangi Selengia wa uruka wa mkuu aliambiwa kutawala Shimbi na hivyo Shimbi ukapoteza hesma ya Umangi rasmi mpaka utawala wa kimangi ulivyokoma baada ya Uhuru. Pamoja na kuwepo kwa Wana wengine wa Mzee Mashelle waliokuwa na uwezo wa kutawala Kama mzee stameza na Karufu njama ilifanywa ili kulinganisha uruka wa Shimbi na Mkuu(kirya) 

SHIMBI NDANI YA UTAWALA WA MABAVU

Baada ya Mangi Selengia kupewa utawala wa shimbi alichagua wasaidizi ambao waliitwa wachili. Alimteua Alli ambaye ndiye aliye laghai pesa za Kodi kwa Mangi Leina Hadi kufukuzwa Umangi, Ali lichukiwa na wananchi wa shimbi kutokana na utawala mbaya.

Katika utawala wa Alli alihakikisha hapati upinzani kwa watoto na wajukuu wa mzee Mashelle kwa kuwaandikisha kujiunga na jeshi la mkoloni miongoni mwao Ni Cosma (Kashomba ) ngalu (Stamesa) William Leina n.k


SHIMBI YABADILISHWA JINA

Mchili Ali alibafili jina la Shimbi katika uongozi wake na kuiita Mwateni , Ali aliendelea kutawa Shimbi mpaka macho yake yalipo koma kuona Tena na baadaye wananchi wa shimbi walimchagua mzee Baiseli Marenga kiwango ambaye alitawala vizuri na heshima ya Shimbi ilianza kufufuka Tena  kwa Sasa Shimbi inatawaliwa na uongozi wa kawaida wa nchi nzima ya Tanzania chini ya maaafisa watendaji wa kata na vijiji.

Umeandikiwa na kudondolewa na 

Emanuel Gasper Kisawani Mashelle

0766605392

Rejeleo A.Abeid&J.W.L. Mashelle (1997) Historia Mila na utamaduni. Head secretarial services. Barabara ya sokoine . Arusha-Tanzania