KWA WALIMU WOTE

Sikilizeni wimbo huu:

Nilipokuwa mtoto niliitwa Chacha

Kwa matamshi yangu ya sasa

 Nilipokuwa kijana niliitwa Chaupele

Nilipokuwa mtu mzima niliitwa Manywele Nilipokuwa mwalimu nikaitwa Bure.

Huu utakuwa wimbo wako

Utakapostaafu urudipo nyumbani Umelewa kangara na nyayo zako

Zikishidwa kulenga njia nyembamba vijijini

Utakuwa kichekesho kwa watoto watakao kuita Ticha popote upitapo

Kumbuka mwalimu utakapostaafu.

Mijusi watataga mayai ndani ya viatu Vyako vilivyokwisha visigino


Na ndani ya sidiria chakavu Zilizoshikizwa kamba kwa pini. Mende watazaliana ndani ya chupa tupu

Za marashi na za bia

Na manyigu yatajenga ndani ya kofia Zilizosahaulika kutani.


Utakapokufa nge watazaliana

Chini ya jiwe juu ya kaburi lako, Na mlevi fulani akipita atapenga

Na kupangusa vidole kwenye jiwe pweke. Mwanzo na mwisho wako ndio huo