Hizi hapa Dalili za mimba changa

Je unajisi kwamba una dalili za mimba changa na huna uhakika? Njia pekee ya uhakika ni kufanya kipimo ndipo utajua mbivu na mbichi. Kabla ya kupima kuna dalili za awali ambazo waweza kuzitumia kukupa mwanga kwamba tayari una ujauzito.
Je Kila Mwanamke anaweza Kupata dalili za mimba mapema?
Kila mwanamke anatofautiana na mwingine kimaumbile. Kuna wengine hawapati dalili kabisa hata mimba ifike miezi mitano. Lakini kuna wanawake wengine huona dalili mapema sana mimba ya miezi mwili tu.
Usichanganye hedhi na mimba
Wanawake wengi hushindwa kugundua mapema kama wana mimba kwasababu dalili nyingi za mimba hufanana na zile za kwenye hedhi mfano kizunguzungu na uchovu.
Dalili zifuatazo zitakupa mwanga iwapo tayari mimba imeingia, japo watakiwa kufahamu kwamba dalili hizi pia zaweza kuwa matokeo ya swala lingine la kiafya. Vipimo ni muhimu kufanyika ili kuwa na uhakika zaidi.
Na kumbuka muda mzuri wa kupima mimba kwa mkojo, ni wiki moja baada ya kuvusha hedhi. Endapo hedhi umpitiliza, ndipo subiri wiki ukapime UPT, utapata majibu sahihi zaidi.
Dalili za Mimba Changa ni hizi
1.Kupata matone ya Damu nyepesi
Baada ya mimba kutungwa yai lililorutubishwa hujishikiza kwenye ukuta wa kizazi. Kitendo hichi kinaweza kupelekea kutokwa na matone mepesi ya damu ukeni na maumivu kwa mbali ya nyonga. Damu hii huitwa implantation bleeding, inatokea siku 6 mpaka 12 baada ya mimba kutungwa.
2.Maumivu kwa mbali ya Nyonga
Maumivu ya nyonga kutokana na mimba changa yanaweza kufanana na yale hedhi. Wanawake huchanganya hilo na kudhani ni hedhi inaanza. Pamoja na kupata bleed nyepesi mwanamke anaweza kuona uchafu mweupe kama maziwa ukeni. Hiki ni kiashiria cha kuanza kuongezeka kwa ukuta wa kizazi ili kushikilia vyema kiumbe kilichotungwa.
Kumbuka uchafu waweza kuendelea kutoka wakati wote wa ujauzito hilo lisikupe mashaka. Lakini kama uchafu utakuwa na harufu mbaya, unaleta muwasho na kujikuna hapo unahitaji kuonana na daktari mapema iwezekanavyo. Kwani waweza kuwa na fangas au maambukizi ya bakteria ukeni.
3.Kubadilika Kwa Matiti
Mabadiliko ya matiti ni moja ya kiashiria kwamba tayari una ujauzito. Kutokanana mabadiliko ya homoni , matiti yanaweza kukua na kujaa week moja baada ya kushika mimba. Matiti pia yanaweza kuwa mazito kuliko kawaida na eneo la chuchu kuwa na weusi zaidi.
Ukiona dalili hizi usiwe na hofu, tambua tu kwamba matiti yataendelea kukua ili kujiandaa kunyonyesha.
4.Uchovu na Kuishiwa Nguvu
Moja ya dalili kubwa ya mimba changa ni kuhisi kuchoka na kusinzia ovyo. Mwanamke huanza kupata dalili hizi wiki moja baada ya kushika ujauzito. Kwanini hali hii itokee? ni kwa sababu ya kuongezeka kwa homoni ya progesterone.
Ukipata dalili hii hakikisha unapata muda mwingi wa kupumzika. Kula zaidi vyakula vya protini na madini chuma.
5.Kichefuchefu(morning sickness)
Kisababishi kikubwa cha kichefuchefu kwa mimba changa haijulikani lakini mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito inaweza kuchangia. Kichefuchefu yaweza kukupata muda wowote, na kuhisi kutapika, japo kwa wengi hutokea zaidi asubuhi.
Baadhi ya wanawake hushindwa kula baadhi ya vyakula baada ya kupata mimba. Hali hii huchangiwa zaidi na mabadiliko ya homoni. Inawezekana kabisa hali hizi za kuchagua chakula, kichefuchefu ikamuandama mwanamke katika siku zote za ujauzito mpaka pale atakapojifungua.
Hakikisha unakula lishe nzuri kila siku ili kumpa mtoto virutubisho vyote vinavyohitajika.
Kukosa Hedhi ni Dalili ya Mimba Changa
Dalili kubwa iliyo wazi ya kwamba tayari una ujauzito ni kupitisha hedhi. Japo siyo kila ukikosa hedhi ni mimba changa hapana. Unaweza kukosa hedhi kutokana na mabadiliko ya homoni, kuongezeka uzito ama kupungua kupita kiasi, mwili kuchoka sana, matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba .
Ukikosa hedhi zaidi ya week mbili ulizozoea, basi hakikisha unanunua kipimo na kupima mkojo kujua kama mimba ipo.
Dalili zingine ya Kuonesha una Mimba Changa
Kukojoa mara kwa mara: Kwa wanawake wengi hali hii huanza baada ya week 6 mpaka 8 ukishika mimba. Lakini kumbuka dalili hii yaweza pia kusababishwa na UTI na kisukari, muhimu kupima.
Kukosa choo ama kupata choo kigumu: kutokana na mabadiliko ya homoni, chakula hupunguza kasi ya kupita kwenye utumbo mdogo. Kupunguza tatizo hakikisha unakunywa maji ya kutosha, fanya mazoezi na kula vyakula visivyokobolewa na vya kambakamba kwa wingi.
Kubadilika kwa mood yako; hasa katka miezi mitatu ya mwanzo
Maumivu ya kichwa na mgongo,inatokea zaidi kwa wanawake wengi wenye ujauzito
Fahamu kwamba mwanamke mjamzito anaweza kuwa na dalili zote hizi ama akawa na dalili baadhi. Kama moja ya dalili hizi itakuboa na kukufanya ujisikie vibaya, ongea na daktari wako atakupa ushauri vizuri.
Comments
Post a Comment