NAFASI ZA KAZI TAKUKURU 2023
Taasisi ya kupambana na Rushwa Takukuru imetangaza nafasi za kazi 2023, Nafasi hizo zilizotangazwa kufuatia tangazo lililotolewa na Takukuru ni maofisa upelelezi nafasi 220 na nafasi 100 za wapelelezi wasaidizi daraja la tatu.
Tangazo hili limekuja ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Polisi kutangaza nafasi 500 za ajira na watu 50,000 kujitokeza kuwania nafasi hizo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Takukuru leo Jumamosi, Januari 21, 2023, waombaji wa nafasi ya maofisa upelelezi wanatakiwa kuwa na Astashahada au shahada ya kwanza katika kozi ya uhandisi, usanifu, sayansi ya kompyuta, sheria na saikolojia.
Kwa upande wa wapelelezi wasaidizi daraja la tatu, wanaohitajika ni waliohitimu elimu ya sekondari na mafunzo yoyote yanayotambulika ikiwemo ya ufundi kutoka katika taasisi zinazotambulika.
Mwisho wa kutuma maombi ni Februari 10, 2023.
Comments
Post a Comment