Nyota wa Yanga na Timu ya Taifa ya Uganda Khalid Aucho

KIUNGO nyota wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Uganda “The Cranes” Khalid Aucho yupo mbioni kutimka mitaa ya Twig ana Jangwani baada ya kugoma kusaini mkataba mpya.

 

Taarifa zilizothibitishwa na chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Yanga zimebainisha kuwa Aucho amegoma kusaini mkataba mpya kwa sababu amepata ofa nono kutoka klabu moja inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Saudi Arabia.

Aucho amegoma kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Yanga

Ikumbukwe mkataba wa Aucho unamalizika mwisho wa msimu huu na tayari mabosi wa Yanga wameendeleza jtihada zao za kumshawishi nyota huyo kubakia Jangwani.

 

Akiwa na Yanga Aucho ameisaidia timu hiyo kupata ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya 28 baada ya kumaliza utawala wa Simba SC uliodumu kwa zaidi ya misimu minne mfululizo.