WANAWAKE wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.

 

Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi.

 

Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote.

 

Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama:

*Vyakula feki (Junk food)

*Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi

*Kutokunywa maji ya kutosha kila siku

*Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala

*Kukaa masaa mengi kwenye kiti

*Kutokujishughulisha na mazoezi

*Mfadhaiko (stress)

*Kula wali kila siku

*Ugali wa sembe

*Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)

Vyakula 25 vinavyoondoa mafuta kwenye tumbo kwa wanawake

 

  1. ASALI NA LIMAU

Chukua asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula na majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili, changanya hivi viwili ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya uvuguvugu na unywe yote mara tu ukiamka asubuhi.

Tumia kwa wiki 3 hivi mpaka mwezi mmoja na hutachelewa kuona tofauti.

 

  1. MAJI YA UVUGUVUGU

Kunywa maji ya uvuguvugu kama lita 1 hivi wakati tumbo likiwa tupu hasa asubuhi ukiamka tu. Hii inasaidia kusafisha mwili na kuondoa mafuta yasiyohitajika.

 

  1. NYANYA

Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na utaona mabadiliko.

 

  1. TANGAWIZI

Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipowe kidogo, ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

 

  1. SIKI YA TUFAA

Siki ya tufaa (apple cider vinegar) inasaidia kupunguza njaa na kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu.

Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha siki ya tufaa mara 1 kwa siku kila siku wakati unakula chakula cha usiku. Kazi nyingine ya hii siki ni kuweka sawa damu sukari mwilini hivyo ni nzuri pia kwa wenye kisukari.

 

  1. MAJANI YA BIZARI

Majani ya bizari husaidia kuondoa sumu na takatka nyingine mwilini kitu ambacho moja kwa moja hupelekea mlundikano mdogo wa mafuta katika tumbo. Kunywa chai ya majani ya bizari kila siku asubuhi, ukikosa majani unaweza kutumia hata unga wake.

 

  1. ILIKI

Iliki hufanya kazi ya kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na ni dawa nzuri sana ya kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini. Iliki pia hutumika katika kupunguza uzito. Tengeneza chai yenye iliki kila siku ndani yake, pia ni kiungo karibu kwa vyakula vingi hivyo hakikisha unaiweka katika kila chakula unachopika kwa matokeo mazuri zaidi.

 

  1. MDALASINI

Mdalasini hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini. Chukua kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na uweke ndani ya glasi 1 ya maji ya moto na uache kwa dakika 5 hivi. Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi ndani yake na ukoroge vizuri, kisha unywe huo mchanganyiko wote asubuhi ukiamka tu.

 

  1. JUISI YA LIMAU

Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.

 

  1. KITUNGUU SWAUMU

Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo (chop) punje 3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili asubuhi tu na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali. Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa haraka zaidi.

 

  1. TIKITI MAJI

Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.

  1. MAHARAGE

Kula maharage kila mara kunasaidia kupunguza mafuta katika tumbo. Maharage yana kiasi kingi cha nyuzinyuzi (faiba) kitu kinachosaidia tumbo lako kutojisikia njaa na hivyo itakuwezesha kula chakula kiasi kidogo.

Kadri unavyokula chakula kichache ndivyo unavyokuwa mbali na uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi tumboni.

Basi kula maharage kila siku.

 

  1. TANGO

Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.