jinsi ya kutoa mimba


Inashauriwa kujua umri wa mimba hiyo. Itakusaidia kupanga hatua zijazo.
Pia inashauriwa kumtaarifu mwenza wako ili ajiandae kisaikolojia na kiuchumi.
Kaa karibu na msaikolojia wako.


Dar es Salaam. Licha ya njia za uzazi wa mpango kuwepo na kutangazwa kila siku, bado mimba zisizotarajiwa ni changamoto miongoni mwa vijana wa Tanzania na dunia kwa ujumla.
Kwa baadhi, habari za kuwa “nina ujauzito” zinaweza kuwafanya watamani dunia iwameze wapotee lakini hakuna haja ya “kupaniki” pale unapopata habari za mimba ambayo ulikuwa haujaipangia.
Badala ya kuanza kuwaza mambo mengi na kutaka kufanya mambo ambayo unaweza kujutia maishani, unaweza kuzingatia mambo haya pale unapopata ujauzito ambao haujaupanga.
Ni pamoja na kumshirikisha mwenzi wako ili kumpatia muda wa kujiandaa na malezi ya mtoto ajaye. 
Kama ujauzito huo unakupa mawazo sana, unaweza kuonana na mtaalamu wa masuala ya afya ili kupata msaada wa kitalamu na kisaikolojia pia.      Pia unaweza kuwajulisha wazazi wako kwani wana uzoefu kuliko wewe.