WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA SUDANI AMEFARIKI KWA CORONA

 


Waziri mkuu wa zamani wa Sudan, Sadiq al-Mahdi amefariki dunia kutokana na virusi vya corona.Mwanasiasa huyo amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mahdi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 84, ndiye waziri mkuu wa mwisho wa Sudan kuchaguliwa kidemokrasia kabla ya kuondolewa madarakani mwaka 1989 kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyomuingiza mamlakani rais wa zamani Omar al-Bashir.

Chama chake cha Umma chenye siasa za wastani, kilikuwa moja ya vyama vikubwa vya upinzani na Mahdi alisalia kuwa kiongozi mwenye ushawishi.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?