Anaitwa James Ngugi, alizaliwa Mwaka 1938 Januari , mji wa Kiambu nchini Kenya .Alizaliwa kipindi cha mwanzoni mwa vita ya pili ya Dunia, na akakulia kipindi cha machafuko ya MAUMAU.

wazazi wake na ndugu zake kama Good Wallance waliwahi kupigana upande wa Muingereza kipindi cha vita ya pili, na pia kipindi cha maumau familia yake ilikamatwa na kuteswa, Kaka yake Mwangi alijiunga na kikundi  Cha Kenyan land and Freedom Army dhidi ya wakoloni , mama yake alikamatwa na kuteswa .

Ngugi elimu yake ameipatia Alliance High School na chuo cha Makerere .

Ngugi wa Thiong'o ni muandishi mashuhuri na mwana utamaduni wa kiafrika, alibadili jina lake la upatizo JAMES NGUGI akidai ni jina la kikristo na la kikoloni na hivyo akajiita NGUGI WA THIONG'O, na vitabu vyake vingi amekuwa akiandika kwa Lugha ya Gikuyu au kiswahili, wazungu wanamuuliza kwanini anaandika kwa GIKUYU kwa niaba ya wa Afrika tuu , yeye anajibu kwanini hawaulizi wao wanapoandika kwa lugha yao, vitabu vyake vingi vimetafiriwa kwa lugha 30(targeted language) kutoka lugha ya GIKUYU(original language).

Ngugi wa THIONG'O, anaamini kuwa "RESISTANCE IS THE BEST WAY TO BE ALIVE" kuwa Ukinzani ndio njia bora ya kuendelea kuishi.

Alianza safari yake ya kuandika vitabu vingi , Riwaya, Tamthilia kipindi cha uongozi wa DANIEL ARAP MOI , kipindi alichokuwa kama makamu wa Rais ,1967 ndio alianza kuandika vitabu vingi sana , vingi vikiwa vinamkosoa na kumchallenge na mambo mengine.

Mfano wa vitabu vyake.
*Weep not child.
*A Grain of wheat 1967.
*petals of blood ,1977

*This Time tommorow 1970, akielezea maisha magumu ya wapigania uhuru , Maumau, na walivyotelekezwa baada ya uhuru.

*Trial of Dedan kimathi 1976.

*I will marry when l want (Ngaahika Ndeenda) 1977, hiko ndiko kitabu ambacho kilimkasirisha Arap Moi ni kipindi ambacho Moi ni makamu wa Rais, Mwaka huo huo Ngugi alikamatwa saa nane za usiku bila kuambiwa kosa lake (Arrested without charges/trials). na kuwekwa katika Gereza la KIMITI MAXIMUM SECURITY PRISON , akiwa huko ndani alitumia karatasi za toilet(Toilet papers) na kalamu ambayo  , walikuwa wakificha juu ya Dari na vitu vingine kama bakuli , sahani aliandika kitabu kingine kiitwacho THE DEVEL ON THE CROSS (caitaani Mutharaba ini).sababu aliamini hawezi ishi bila kuandika na hajui atatoka lini huko sababu alikamatwa bila mashtaka wala kosa kuambiwa.

1978 ,aliachiwa na kipindi hiko ndicho ambacho Daniel ARAP MOI aliingia kuwa Rais kutoka makamu wa Rais, alifukuzwa kuwa professor wa chuo cha NAIROBI na famila yake ilipitia mateso na manyanyaso kutokana na maandishi yake na kalamu yake ya kukemea uovu kwa jamii.

Ngugi wa THIONG'O alilazimishwa na kufukuzwa nje ya Nchi kwenda kuishi uhamishoni marekani na uingereza ,na kwa muda wote wa urais wa Moi haikuwa salama yeye kurudi hadi miaka 22 baadaye ambapo ni 2002 , Arap moi alipotoka madarani ndio ilikuwa salama kwake kufikiri kurudi ila hakuwahi rudi kuishi Kenya.

Akiwa uko nje uhamishoni aliendelea kuandika vitabu kama DECOLONIZING the mind ,1981, na writer's prison Diary .

2004 ,tar 8 August  alirudi Kenya kwa matembezi ,wakiwa katika Apartment fulani waliyofikia yeye na mke wake ,wavamizi walitambulika kama  (ROBBERS) walivunja na kumvamia (Assaults) na wakamdhalilisha mke wake (sexial Assault) na kumuibia vitu vingi vya thamani .

Ngugi aliporejea tena Marekani aliandika kitabu kiitawacho Wizard of Crow (Murogi wa Kagogo).

Mwaka 2006 ,November 10 mmiliki wa hotel aliyokuwa akiishi Ngugi wa THIONG'O huko SAN Fransisco alimuamuru aondoke ,ila watu wengi diaspora ,wazungu na wa Afrika walipinga na kumtetea .

Hadi sasa Ngugi wa THIONG'O bado anaishi huko nje ,sasa ni muandishi mashuhuri kimataifa ,ameapa kutoacha kuandika sababu anapaswa kuandika dhidi ya uovu au jambo lolote .

Amewahi tunukiwa Tuzo mbalimbali za uandishi bora ,na sasa ni Mhadhiri wa vyuo tofauti huko Marekani na uingereza,amekuwa akitoa wito kwa waandishi wa Afrika kuepuka uandishi wa kujitengenezea fedha ila uandishi dhidi ya maovu ya serikali zao ili kusaidia jamii..


© Mashauri Vicent