Kwa mujibu wa Wafula (1999) ni utungo wa kisanaa ambao huweka wazo fulani katika matendo na mazungumzo nae Mlama (2003), neno tamthiliya limetumika kwa maana ya kile ambacho wengine hukiita “michezo ya kuigiza’’. Tamthiliya ni utungo wa drama ambao ni moja ya maandishi ya sanaa za maonesho. Anaendelea kusema “ sanaa za maonesho hapa ichukuliwe kwa maana ya sanaa ambayo huwasilisha ana kwa ana, tukio fulani kwa hadhira kwa kutumia usanii wa kiutendaji’’. Kwamfano badala ya kuliwasilisha wazo kwa hadhira kwa kutumia maneno kama ilivyo katika ushairi, sanaa za maonesho huliweka wazo katika hali ya tukio linaloweza kutendeka kwa kutumia usanii wa utendaji kama vile vitendo na uchezaji.
Kwa ujumla tamthiliya ni kazi ya fasihi ambayo hukusudiwa kuwasilishwa kupitia njia ya maandishi na matendo ya wahusika ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira husika.
2.0 Chimbuko na historia ya Tamthiliya ya Kiswahili
Mulokozi (2017) anaeleza chimbuko na historia ya Kiswahili katika vipindi vinne vya kihistoria yaani kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni, kipindi cha uhuru. Anaeleza kuwa kabla ya ukoloni tamthiliya zilizoandikwa hazikuwepo  badala yake zilikuwepo drama zisizoandikwa ambazo zilikuwa na sifa za tamthiliya yaani hadithi, vitendo waigizaji na dialojia.Mfano mzuri wa drama hizo ni maigizo ya watoto wanapoigiza maisha ya unyumba huwa wanamithilisha maisha halisi ya jamii.
Wakati wa ukoloni, tamthiliya halisi inayoeleweka kwa vigezo vya kifasihi imetokea wakati huu; ambayo ililetwa na wakoloni kutoka ulaya katika kipindi cha miaka ya 1890 na kumalizika miaka ya 1960. Katika kipindi hiki kulikuwa na aina mbili za tamthiliya, yaani tamthiliya ya kizungu iliyolenga kuwaburudisha maafisa wa kizungu na kujifunza Biblia kupitia vikundi vya kuigiza kama vile Dar es salaam players ( 1947) na Arusha little theatre (1953) na aina ya pili ilikuwa tamthiliya za vichekesho. Tamthiliya hizi zililenga kuchekesha, kuwasuta watu waliofikiriwa kuwa washamba au wasiostaarabika.  Hizi zilianza kuchapishwa mwaka 1950, ambapo 1951 ilichapishwa tamthiliya ya T. Frank iliyoistwa imekwisha.
Kipindi cha uhuru, tamthiliya za kizungu zilipoteza umaaarufu wake hasa kwa upande wa Tanzania baadhi ya tamthiliya za kizungu ziliafsiriwa ili wananchi wapate kuzielewa, mfano Juliasi Kaizari ( 1964) na Mabepari wa Venis. Baada ya uhuru tamthiliya nyingi za wakati huo zilihusu wazungu weusi, Waafrika waoringia elimu, vyeo na kusahau utamaduni wao. Tamthiliya zilizochapishwa kipindi hiki ni Wakati ni ukuta ya E. Hussein.
2.1Mikondo ya Tamthiliya ya Kiswahili
Kwa mujibu wa Mulokozi (2017), historia na chimbuko la tamthiliya ya Kiswahili inaweza kufafanuliwa vizuri kwa kutumia mikondo mbalimbali. Ifuatayo ni mikondo ya tamthiliya ya Kiswahili kwa mujibu wa mtaalamu Wafula (1999) na Mulokozi (2017).
2.1Migogoro ya Tamaduni
Katika kipindi hiki tamthiliya zilijikita katika kuonesha mvutano uliokuwepo katika maisha ya mijini na maisha ya vijijini, utamaduni wa Mwafrika na utamaduni wa kigeni hasa ule wa kimgharibi Wafula (1999). Mifano ya tamthiliya hizo ni Wakati  Ukuta iliyoandikwa naE. Hussen ( 1967), Hatia iliyoandikwa na P. Mhando (1972), na Uaisi iliyoandikwanaJ. Kitsao(1980).
2.2 Matatizo ya Kijamii  
Mulokozi (2017) anainisha matatizo ya kijamii kuwa ni mapenzi, ndoa, ufukara na urithi. Anaeleza kuwa tmthiliya nyingi ziliandikwa zilizungumzia mambo hayo katika jamii, mifano ya tamthiliya hizi ni Nakupenda lakini ya F. Topan (1971) na Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi iliyoandikwa na G. Ngugi (1961). Aidha tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe inalitazama suala la mapenzi katika muktadha wa utumishi wa umma na kuonesha kuwa mapenzi huweza kuathiri uwajibikaji katika kazi, vilevile tamthiliya ya Pambo iliyoandikwa na P. Mhando inaonesha suala la elimu na dhima yake katika jamii.
2.3 Tamthiliya na Itikadi
Wafula (1999) anasema kwa hakika baadhi ya tamthiliya za kiitikadi zilihusu masuala ya mashujaa wa Kiafrika vilevile zilihusu masuala ya kiuchumi na kisiasa kwa kuzingatia misingi ya ujamaa. Tamthiliya hizo ni pamoja na Kinjikitile iliyoandikwa na E. Hussein, Mkwava wa Uhehe iliyoandikwa na Mulokozi. Aidha katika itikadi masuala ya dini na itikadi za kijadi ipo tamhiliya kadhaa kama Ngoma ya Ngw’anamalundi  iliyoandikwa na E. Mbogo, Njia panda iliyoandikwa na Muhanika na nyinginezo.
2.4 Ukombozi wa Taifa na Ujenzi wa Jamii mpya
Mulokozi (2017) anadai kuwa masuala haya yamejitokeza katika tamthiliya nyingi, ambapo watunzi waliangalia suala laukombozi katika muktadha wa ukoloni wanasawiri harakati za upinzani dhidi ya ukoloni, ukombozi wa taifa na suala la haki, mifano ya tamthiliya hizo ni Harakati za ukombozi iliyoandikwa naP. Mhando,  N. Balisidya na Lihamba na tamthiliya ya Tambueni Haki zetu iliyoandikwa na Mhando. Kwaupande wa ujenzi wa jamii mpya tamthiliya zilikuwepo ni pamoja na Mashetani  iliyoandikwa na  E. Hussein, Giza limeingia ya Mbogo. Pia suala la udikteta lilishamiri katika jamii nyingiza Kiafrika lilishambuliwa kisanaa katika tamthiliya kama Kaptula la marx iliyoandikwa na E. Kezilahabi akishutumu matumizi mabaya ya madaraka katika mfumo wa ujamaa ulioanzishwa na Nyerere .
2.5 Matatizo ya Kijinsia
Masuala ya kijinsia pia yaliwashughulisha watunzi wengi wa tamthiliya ya Kiswahili, ambapo watunzi wengi walijaribu kuonesha hali duni ya mwanamke katika jamii ya sasa na kutafuta sababu hali hiyo na kupendekeza ufumbuzi. Baadhi ya tamthiliya hizo ni Nguzo Mama iliyoandikwa na P. Mhando, Machozi ya mwanamke  iliyoandikwa na Ngozi na Tone la Mwisho iliyoandikwa na E. Hussein.
3.0 Historia na Chimbuko la Tamthiliya ya Ulaya
Historia na chimbuko la tamthiliya ya Ulaya inaweza kufafanuliwa katika vipindi tofauti tofauti kama ifuatavyo.
3.1 Kipindi cha Kuanguka kwa Ngome (utawala) ya Warumi
Tamthiliya barani Ulaya zilianza baada ya kuanguka kwa ngome (utawala) ya  Warumi, ambapo makundi ya watu wachache yaliundwa na kuigiza mbele ya hadhira . Maudhui ya maigizo hayo yalijikita katika kuburudisha hadhira lengwa.
3.2 Kipindi cha Utawala wa Makanisa
Baada ya kipindi cha kuanguka kwa utawala wa Warumi kilikuja kipindi cha utawala wa makanisa au mvumo wa makanisa ambapo mojawapo ya huduma zilizotolewa ilitwa “ The hours” . Katika huduma hiyo maandiko ya kwenye Biblia yalikuwa yanaigizwa yakiambatana na muziki. Tamthiliya ya kwanza kuandikwa iliitwa Concordia iliyoandikwa na Ethel Wold ambaye alikuwa kiongozi wa kanisa la Winchester.
3.4 Kipindi cha Zama za Kati
Hadi kufikia karne ya 14 uandikaji na uzalishaji wa tamthiliya haukuwa tena chini ya makanisa bali wao walibakia kama sehemu ya kurekebisha maudhui ya kile kilichotungwa. Katika kipindi hiki walikuwepo waandishi kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii kama vile wafanyabiashara ambao nao waliandika tamthiliya, mfano huko Englandwafanyabiashara waliandika tamthiliya ya Shipwrights staged the building of Noah’s art. Tamthiliya ambayo ilienda kinyume na sheria za Kirumi za utunzi wa tamthiliya ambapo waliandika kwa kufuata itikadi na tamaduni za makabila yao. Waandishi wengine ni pamoja na Hubert Cailleau (1547) wa Ufaransa aliandika tamthiliya iliyoitwa Valenciennes Mysterty play.
Katika kipindi hiki shirika la uigizaji la Ulayalilipewa nafasi ya kusimamia masuala ya utunzi na mitindo ya tamthiliya. Hadi kufikia karne ya 16 waandishi wengi wa tamthiliya waliibuka kama Shake Spears, aliandika tamthiliya Comedy of Errows, Romeo and Juliet, Juliasi Caesar kama   Thomas Kyol aliandika The Spanish tragedy, Christopher Marlowe aliandika Doctor  Faustus.
4.0 Ulinganishi wa Historia Chimbuko la Tamthiliya ya Kiswahili na Tamthiliya ya Ulaya
Mulokozi (2017) anasema kuwa chimbuko la tamthiliya kote huenda lilichipuka kutokana na mambo makuu matatu, mambo haya yafuatayo;
Kwanza, miviga na viviga ya kijamii na kidini pamoja na misahafu ya kidini, mwanzo tamthiliya za Ulaya zilitokana na matendo ya kijami kama kuzaliwa kwa mtoto, kukua, kuoza na kuzaliwa upya ambako kulihusishwa na mungu wao aliyeitwa Dionizi  vivyo hivyo kwa upande wa tamthilia ya Kiswahili inaelezwa kuwa chimbuko lake ni maigizo ya kijamii kama vile kuzaliwa kwa mtoto, jando na unyago, msiba, arusi ibada za kutambika na kutawazwa kwa mtemi. Hivyo chimbuko la tamthiliya dunia lilitokana na matendo mbalimbali katika jamii husika.
Pili, tamthiliya kote duniani zilitokana na umithilishaji wa maisha ya kawaida kwa ajili ya kutoa elimu, burudani, maonyo au michezo. Tamthiliya zililenga kuelezea maisha halisi ya kila siku pamoja na changamoto zinazopatikana katika jamii husika, umithilishaji wa maisha ulisababisha kuandikwa tamthilia nyingi duniani. Kwa mfano tamthiliya Kinjilitile na Mkwava wa Uhehe zilielezea maisha wakati wa ukoloni na mapambano dhidi ya ukoloni, nyingine zilihusu masuala mengine katka jamii kama vile mapenzi, umaskini na rushwa, mfano tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe ilizungumzia mapenzi na utumishi wa umma.
Tatu,tamthiliya zilitokana na sanaa za maonesho ya kijadi kama vile ngoma na dansi, kwa upande wa tamthiliya za Kiswahili zilitokana na ngoma zilizopigwa kutokana na jambo au tukio fulani  la kijamii na tamthiliya za Ulaya zilitokana na dansi
Aidha tamthiliya zote zimepitia mabadiliko mbalimbali ya kihistoria, tamthiliya za Kiswahili zilizoandikwa ili ziigizwe jukwaani ni matokeo ya athari za tamthiliya za Ulaya. Kutokana na  historia tamthiliya ya Kiswahili zilipitia vipindi kadhaa yaani kabla ya uhuru yamfano imekwisha ya T Frank, wakati wa ukoloni wakati wa uhuru mfano, Julias kaizar na mabepari wa venis na baada ya uhuru mfano wakati ukutailiyoandikwa na E. Hussein vilevile tamthiliya ya ulaya nayo imepitia vipindi mbalimbali vya kihistoria kama vile kipindi cha kuanguka kwa utawala wa Kirumi ( ambapo tamthiliya zilisimama kama maigizo), kipindi cha utawala wa kama The hours  kanisa tunapata tamthiliya  utawala wa makampuni na mwisho ni umiliki na uandishi wa watu binafsi ambapo waliibuka waandishi binafsi kama Shake Spears.
Tamthiliya zote zinafuata kanuni za ki-Aristotle, yaani kwa mujibu wa kanuni za,ki-Aristotle tamthiliya yoyote huwa na vipengele vifuatavyo, hadithi (ganizi au simulizi), vitendo, waigizaji wanaomithilisha wahusika wa hadithi na dialojia (mazungumzo). Athari hizi hutokea katika tamthiliya zote za Kiswahili na Ulaya yaani zote zinafuata kanuni za ki-Aristotle. Kwa mfano tamtliliya ya Nguzo Mama, Kwenye Ukiongo wa Thim na Kivuli Kinaishi zote zimefuata kanuni hizo za Ki-Aristotle, aidha vipengele hivyo vinajidhihirika katika tamthiliya za Ulaya mfano tamthiliya ya Mfalme Edipode na nyinginezo
Licha ya ufanano huo wa chimbuko na historia ya tamthiliya za Kiswahili na Kiulaya lakini pia fasihi hizi mbili zinatofautiana kwa namna mbalimbali kama ifuatavyo;
Tamthiliya za Kiulaya ni kongwe kuliko tamthiliya za Kiswahili, chimbuko na historia ya tamthiliya barani ulaya ilianza tangu kipindi cha dola ya Warumi ambapo kazi ziliandikwa na kuigizwa katika sehemu za wazi kwa kuhusisha vikundi vidogovidogo, Baadae utawala wa makanisa ulichukua nafasi na kazi nyingi zilizohusu biblia ziliandikwa na kuigizwa hadharani mfano wa tamthiliya za mwanzo ni Concordia na maendeleo makubwa yakachukua nafasi katika karne ya 15 tofauti na chimbuko la tamthiliya za Kiswahili katika maandishi zililetwa na wazungu wenyewe kipindi cha ukoloni.
Tamthiliya za Kiswahili zilijikita katika ukombozi, Tamthiliya nyingi za Kiswahili za wakati huo  hasa baada ya uhuru zilijikita katika kupigania ukombozi wa kifikra, ujenzi wa jamii, migongano ya kiutamaduni na kisiasamfano wa kazi hizo ni kama mashetani (1971), KwenyeukingowathimnaLinaubani tofauti na tamthiliya za Kiulaya ambazo nyingi zinazungumzia masuala ya kutokuwapo kwa uhalisia na yale yaliyopo katika jamii mfano; Shipwrightsstagedthebuildingof Noahs art, pia Brecht alianzisha kanuni ya ukengeushi ambayo ambapo alitumia mbinu za utendi, uhistorishaji na nyinginezo kuelezea matukio katika tamthiliya bila kuhusisha na uhalisia wa mambo yaliyopo katika jamii mfano wa kazi zake ni Galileo (1943) na Thegoodwomen ofSetzuan(1943).
Maendeleo ya tamthiliya yamechukua mikondo tofauti kutegemeana na historia na utamaduni wa jamii inayohusika, Mulokozi (2017) anaeleza kuwa ingawa asili ya tamthiliya katika nchi na tamaduni mbalimbali yaelekea kufanana lakini yana maendeleo tofauti kulingana na historia na utamaduni wa jamii, Kwa mfano Wayunani walizigawa tamthiliya katika mikondo miwili ambayo ni tanzia na komedia ambayo kulingana na historia na utamaduni wao tanzia zilihusu mkasa uliomsibu mtu mashuhuri na yanapata msukumo kutokana na udhaifu alio nao na tanzia ziliwahusu watu wa kawaida tofauti na tamthiliya za Kiswahili kutokana na historia na utamaduni wa jamii zimegawanyika katika mikondo saba ambayo ni migongano ya kiutamaduni mfano tamthiliya ya Wakati ukuta na Kwenye Ukingowa Thim, matatizo ya kijamii( kama ndoa, umaskini na ufukara) mfano wa tamthiliya ni Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi,Ukombozi na utaifa mfano Kinjekitile na Mukwava wa uhehe, ujenzi wa jamii mpya mfano kaptura la marx, matatizo ya kijinsia na falsafa ya maisha mfano wa tamthiliya ni Nguzo Mama na  Machoziya Mwanamke na mkondo wa mwisho ni uchawi, uganga na itikadi za jadi mfano wa tamthiliya zilizopatikana hapa ni Ngoma ya Ng’wanamalundi na Kitogobaadae ikafuata na mkondowa majaribio.
Kwa ujumla, licha ya chimbuko na historia ya tamthiliya ya Kiswahili na Ulaya kupiga hatua katika mataifa mbalimbali. lakini pia maendeleo ya sayansi kupitia mchepuo wa filamuzinazooneshwa kupitia televisheni, DvD na video zimesaidiwa kuhifadhi na kuendeleza maarifa.









MAREJELEO
Comtois, E 2nd Edition.The European History of Theatre
Mulokozi, M.M (2017).Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili, Kozi za Fasihi Vyuoni na Vyuo 
                           Vikuu. Dar es Salaam: KATTU
Mlama ( 1983),Utunzi wa Tamthiliya katika Mazingira ya Tanzania. Dar es Salaam: Taasisi ya 
               Uchunguzi wa Kiswahili
Wafula, R.M (1999), Uhakiki wa Tamthiliya. Historia na Maendeleo. Nairobi-Kenya. Jomo
                       Kenyata Foundation