Karibu ndugu msomaji katika makala hii.
Mwandishi
E. G. Masshele

Kwa miaka mingi wataalamu na wadau mbalimbali wamekuwa wakihitilafiana kuhusu muono wa Nguli wa fasihi Guru Ustadh  Shaaban Robert juu ya wanawake katika kazi zake zile za kinudhumu na kinathari. Wengi wakidai mwanafasihi huyu amekuwa sio mtetezi kabisa wa wanawake Bali aliwatazama wanawake kwa namna hasi. Lakini kwanini waseme hivyo wakati ukitalii kazi nyingi za nguli Huyu utaona namna alivyo watetea na kuwachora wanawake katika namna bora kabisa? Pengi wenye mwono wakuwa Shaaban aliwatazama wanawake kwa namna hasi hawakuzielewa kazi zake au pengine hawakupata wasaa wakuzitalii


Katika mfululizo wa makala haya nitakuchambulia kazi moja moja ndiposa, wewe mwenyewe upate mahitimisho.

Diwani : PAMBO LA LUGHA
MWANDISHI: SHAABAN ROBERT
Nairobi Oxford Unversity Press

> Mwanamke anastahili kuheshimiwa. Mwandishi SHAABAN ROBERT anaona nimuhimu kuwaheshimu wanawake na haya yanajidhihirisha katika shairi la "Mwanamke si kiatu" UK 19
anasema

Wanawake wana laana, jibu lako      ufedhuli, lawama lastahili, kuwa hujui kunena, Umchache wa akili, Wanawake bora sana, ni hazina ya awali.


Mwandishi anawapiga vita wanaona Mwanamke ana laana. Bila kusahau kupiga vita dharau juu ya wanawake.


>Mwanamke ni kiumbe mwenye thamani.

Shairi " Mume na make"
 Mwanamke shetani, watu wengine wanena,
Kuja kwake duniani, kuwa ameleta laana,
Nami kwa yakini, Juu ya hili nabishana,
Kuwa anathamani  na mwanaume walingana.

Hapa mwandishi anaona Mwanamke na Mwanamke wana thamani sawa.


 >Mwanamke kama kiumbe muhimu katika maisha.

Shairi "mume namke UK 33

Sura ya kufurahisha, kama ile ya pepo
Inayopamba maisha, duniani tukaapo,,
Kusema yalaanisha, akili yangu haipo,
.............

Shairi la " Peke"
UK 2
Mpenzi wangu mwandani, Tangu nilipoona,
Hali yako taabani, furaha moyoni sina, lepe kupata machoni, La usingizi nakana, poa tuwe furahani, kuishi pekesiwezi.


Shairi "mume na mke"
Mke nyumbani faraja, kushinda mtumishi,
Mshahara huna haja, nakazi haimchoshi, ...............
Uk35

Aidha mwandishi anamtetea Mwanamke pale anapokosea kwa kusema
Shairi "Mume na mke"
Maovu ya Mwanamke, pamoja na mwanaume, mwanaume kazi yake, kumwinua asizame, ............. UK 35.


Pia angalia shairi la "siku tukufu"

Mwanamke kuwa nikiumbe muhimu inajidhirisha pia katika shairi la "Kiswahili" uk27

Titi la mama litamu, hata likiwa la mbwa,....................


Uhakiki huu utaendelea
info.masshele@gmail.com