Kila eneo katika mfumo wa kumeng'enya chakula lina kazi yake maalumu katika umeng’enyaji wa chakula. Baadhi ya haya maeneo kama mdomo, tumbo na utumbo mdogo huwa kuna vimeng’enya mahususi kwa aina maalumu ya chakula kitakachopita; mfano, mdomo humeng’enya vyakula vya wanga na tumbo humeng’enya vyakula vya protini ambapo utumbo mdogo humalizia kazi na kumeng’enya aina zote za chakula.


Je, kuna shida ya mimi kunywa maji au soda wakati wa kula?

Unywaji wa maji au soda huweza kuingilia ufanyaji wa kazi wa mfumo wa umeng’enyaji kwa njia zifuatazo;
·     
    Kupunguza muda wa chakula kukaa tumboni. Kwa kawaida tumbo hutunza chakula ili kiweze kumeng’enywa vizuri na kazi hii huwa na ufanisi kama chakula kitakuwa katika mfumo wa ujiuji. Chakula kikiwa kina kimiminika kwa sana huwezi kupita tumboni kwa haraka bila kumeng’enywa.
·         Kupunguza makali ya asidi iliyoko tumboni. Tumboni kuna asidi ya haidrokloriki ambayo husaidia kuua vimelea vya magonjwa na pia kusaidia vimeng’enya kufanya kazi. Unywaji wa maji mengi huingilia ufanyaji wa kazi wa asidi hii hivyo kupunguza ufanisi wa vimeng’enya.

·         Huepelekea kupata kiungulia. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa ujazo wa asidi baada ya kunywa maji mengi. Hii husababisha asidi hiyo kupanda kwenye koo la chakula na kusababisha hisia hiyo ya kiungulia.

Pia, ukiacha kuwa ni tabia ya kawaida kwa baadhi ya watu kupendelea kunywa maji mengi wakati wa kula, sababu nyingine huwa upikaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi hivyo kuleta kiu, pia ulaji wa haraka haraka ambao husababisha chakula kukwama kwenye umio. Sababu hizi zote husababisha unywaji wa vimiminika wakati wa kula.
Mwisho,Maji yana umuhimu pia katika kumeng'enya chakula.Inashauriwa kunywa maji nusu saa kabla ya kula chakula na nusu saa baada ya kula ili isiathiri Mmeng'enyo wa chakula.