Kumekuwa na nadharia mbali mbali na uelewa tofauti tofauti kuhusu Chimbuko au chanzo cha Virusi vya ukimwi na UKIMWI, wapo walioaminishwa kwamba virusi hivi vimetengenezwa mahususi kuwamaliza wafrika, wapo walioaminishwa kwamba virusi hivi vimetengenezwa na Bwana Richard Gallo kama siraha ya kuwaangamiza maadui wa Marekani, Wapo walioaminishwa kwamba virusi hivi vinatokana na Chanjo ya polio na Kadharika.

Ila niseme tu nadharia hizi si kweli,
Nemeamua kuandika makala hii mahususi kwa ajili ya kuwaelezea chimbuko la VVU na kuwawekea ushahidi wa machapisho na tafiti zilizofanyika miaka hiyo mpaka kupatikana Jina la VIRUSI VYA UKIMWI. Kusoma tafiti hizo na machapisho hayo bofya link znazoonekana kwa rangi ya kijani itakufungulia usome.


UKIMWI ulitambuliwa mara ya kwanza na Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa huko Marekani mwaka 1981, ilhali kisababishi chake - VVU - kilitambuliwa mwanzoni mwa muongo huo nchini huko.


UKIMWI ulitambuliwa mara ya kwanza na Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa huko Marekani mwaka 1981, ilhali kisababishi chake - VVU - kilitambuliwa mwanzoni mwa muongo huo nchini huko.

Kwanza kabisa tufahamu kuwa Virusi hivi kwa nchini Marekani viligunduliwa na kupewa jina la HIV  mwaka 1983,hapo unaweza kuona ni muda gani ulikua umepita baada ya vita ya pili ya duni.
wakati huo huo inasemekana kwa Africa watu walikua tayari wameanza kupata ugonjwa huu tokea mwaka 1900, Fuatna nami katika makala hii kujua waliupata kutokea wapi.

 Gallo RC . "A reflection on HIV/AIDS research after 25 years" (https://retrovirology.biomedcentral.com/articles/10.1186/1742-4690-3-72)
 
Matukio ya kwanza yalikuwa katika kikundi kidogo cha waraibu wa dawa za kulevya za kujidunga kwenye mishipa na wanaume mashoga wasiokuwa na visababishi bayana vya udhaifu wa kingamwili na walioonyesha dalili za aina ya homa ya mapafu inayojulikana kama ya Pneumocystis carinii, maambukizi nyemelezi yanayotokea kwa nadra na maarufu katika watu wenye kingamwili dhaifu sana. 

 Nakala Gottlieb MS (2006). "Pneumocystis pneumonia—Los Angeles. 1981"Am J Public Health 96 (6): 980–1; discussion 982–3.  Archived from the original on April 22, 2009. Retrieved March 31, 2009. Linkhttp://www.cdc.gov/mmwr/preview/mmwrhtml/june_5.htm

Punde baadaye, idadi isiyotarajiwa ya mashoga wakapata saratani inayojulikana kama Kaposis Sarcoma (KS), saratani ya ngozi iliyokuwa nadra sana hapo awali.Visa vingine vingi vya Nimonia aina ya Pneumocyst carnii na kaposis sarcoma vilitokea huku vikitahadharisha Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani, hivyo kikosi cha kiutendaji kikaundwa ili kuudhibiti mzuko huu.

Nakala 
 Basavapathruni, A; Anderson, KS (December 2007). "Reverse transcription of the HIV-1 pandemic". The FASEB Journal 21 (14): 3795–3808 linkhttps://www.fasebj.org/doi/10.1096/fj.07-8697rev

Katika siku za kwanza, kituo hicho hakikuwa na jina rasmi la ugonjwa huu, mara nyingi wakitumia majina ya magonjwa mengine yaliyohusishwa nao, kwa mfano, lymphadenopathy, jina ambalo baadaye wavumbuzi wa VVU waliviita virusi hivi.
 Nakala 
 1. Centers for Disease Control (CDC) (1982)."Persistent, generalized lymphadenopathy among homosexual males"MMWR Morb Mortal Wkly Rep. 31 (19): 249–251

2.Barré-Sinoussi F, Chermann JC, Rey F et al. (1983). "Isolation of a T-lymphotropic retrovirus from a patient at risk for acquired immune deficiency syndrome (AIDS)".Science 220 (4599): 868–871. doi:10.1126/science.6189183 

 Wavumbuzi pia walitumia “Sakoma ya Kaposi na Maambukizi nyemelezi”, jina lililokuwa la kikosi cha kiutendaji kilichoanzishwa mwaka wa 1981.


 Centers for Disease Control (CDC) (1982)."Opportunistic infections and Kaposi's sarcoma among Haitians in the United States"MMWR Morb Mortal Wkly Rep. 31 (26): 353–354; 360–361. PMID 6811853 . Retrieved August 31, 2011. 

Wakati mmoja, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kiliunda msemo "ugonjwa wa 4H", kwani tatizo ili  lilionekana kuwaathiri watu wa Haiti, mashoga (homosexuals), wenye tatizo la hemophilia na watumiaji wa heroini. Katika vyombo vikuu vya habari liliundwa neno "GRID" (lililosimamia "gay-related immune deficiency", yaani "ukosefu wa kinga uliohusishwa na mashoga"

  Altman LK. "New homosexual disorder worries health officials", The New York Times, May 11, 1982. Retrieved on August 31, 2011.

  Hata hivyo, baada ya kutambua kuwa VVU havikuwaathiri jamii ya mashoga pekee, ilibainika kuwa neno GRID lilikuwa likipotosha, hivyo neno UKIMWI likaanzishwa kwenye mkutano mnamo Julai 1982.Kufikia Septemba 1982, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kilianza kuuita UKIMWI.

 Kher U. "A Name for the Plague", Time, July 27, 1982. Retrieved on March 10, 2008. Archived from the original onMarch 7, 2008. 

Centers for Disease Control (CDC) (1982). "Update on acquired immune deficiency syndrome (AIDS)—United States". MMWR Morb Mortal Wkly Rep. 31 (37): 507–508; 513–514. PMID 6815471
  

Robert Gallo, mzinduzi mwenza wa VVU katika miaka ya kwanza ya 1980, akiwa pamoja na (kushoto kwenda kulia) Sandra Eva, Sandra Colombini, na Ersell Richardson.

Mnamo 1983, vikundi viwili tofauti vya watafiti vilivyoongozwa na Robert Gallo na Luc Montagnier bila kutegemeana vilitangaza kuwa kirusi aina Retrovirus kipya kiilikuwa kikiwaambukiza wagonjwa wa UKIMWI, hivyo wakachapisha matokeo yao katika jarida la Science.

 RC Gallo, PS Sarin, EP Gelmann, M Robert-Guroff, E Richardson, VS Kalyanaraman, D Mann, GD Sidhu, RE Stahl, S Zolla-Pazner, J Leibowitch, and M Popovic (1983). "Isolation of human T-cell leukemia virus in acquired immune deficiency syndrome (AIDS)". Science 220 (4599): 865–867. doi:10.1126/science.6601823 .PMID 6601823 

Gallo alidai kuwa virusi vilivyokuwa vimetambuliwa kwa mara ya kwanza na kikundi chake kilikuwa sawa katika umbo na seli za binadamu. Kikundi cha Gallo kiliviita virusi hivi HTLV-III.

Wakati huohuo, kikundi cha Montagnier kilitambua virusi kutoka kwa mgonjwa aliyekuwa na uvimbe wa tezi za limfu kwenye shingo na udhaifu wa mwili ambazo ni dalili mbili bainifu za UKIMWI. Huku wakikanusha ripoti ya kikundi cha Gallo, Montagnier na wenzake walionyesha kuwa viini vya protini vya virusi hivyo vilikuwa tofauti na HTLV-I kiukingamwili. Kikundi cha Montagnier kiliviita virusi walivyovitambua virusi vinavyohusishwa na kuvimba kwa tezi za lymph yaani Lympadenopathy. Virusi hivi vilibainika kuwa sawa mwaka wa 1986 na kubadilishwa na kuitwa VVU.

 Basavapathruni, A; Anderson, KS (December 2007). "Reverse transcription of the HIV-1 pandemic". The FASEB Journal 21(14): 3795–3808. doi:10.1096/fj.07-8697rev .PMID 17639073
  
Aina za Virusi vya UKIMWI zinazopatikana Africa yaani  VVU-1 na VVU-2 vimetokana na jamii ya sokwe wa asili ya huko Afrika Magharibi na ya Kati mwishoni mwa karne ya 19 au mwanzoni mwa karne ya 20, wakati virusi vya Simian Immunodeficiency virus SIV kutoka kwa nyani au sokwe vilikwenda kwa binadamu.VVU-1 vinaaminika kutoka kusini mwa Cameroon kupitia kugeuka kwa VSVU(cpz) Vilipoingia mwilini mwa binadamu , (virusi vya sokwe vinavyosababisha ukosefu wa kinga mwilini) vinavyoambukiza sokwe wa mwituni (VVU-1 hutokana na mzuko wa magonjwa ya VSVUcpz katika jamii ya sokwe iitwayo Pan troglodytes troglodytes).Watu walipata virusi kupitia tabia ya kushika na kula nyama mbichi wakati mwingine damu za wanyama walioathirika kugusana na majeraha yao hivyo virusi hivi kuweza kuingia kwenye miili yao.
 
 Gao F, Bailes E, Robertson DL et al. (February 1999). "Origin of HIV-1 in the chimpanzee Pan troglodytes troglodytes".Nature 397 (6718): 436–41.doi:10.1038/17130 . PMID 9989410

 Keele, B. F., van Heuverswyn, F., Li, Y. Y., Bailes, E., Takehisa, J., Santiago, M. L., Bibollet-Ruche, F., Chen, Y., Wain, L. V., Liegois, F., Loul, S., Mpoudi Ngole, E., Bienvenue, Y., Delaporte, E., Brookfield, J. F. Y., Sharp, P. M., Shaw, G. M., Peeters, M., and Hahn, B. H. (28 July 2006). "Chimpanzee Reservoirs of Pandemic andNonpandemic HIV-1". Science 313 (5786): 523–6. doi:10.1126/science.1126531 .PMC 2442710 . PMID 16728595
Link : https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/16728595
  
Virusi vinavyohusiana kwa karibu na VVU-2 ni VSVU(smm) ambavyo ni virusi vya nyani aina ya Cercocebus atys atys, tumbili wa kale anayeishi Afrika Magharibi (kutoka kusini mwa Senegali hadi magharibi mwa Côte d'Ivoire). 

 Reeves, J. D. and Doms, R. W (2002). "Human Immunodeficiency Virus Type 2". J. Gen. Virol. 83 (Pt 6): 1253–65. doi:10.1099/vir.0.18253-0 . PMID 12029140

Tumbili wa kisasa kama vile tumbili bundi wana ukinzani wa maambukizi ya VVU-1 kwa sababu ya kuwa na uunganishaji wa Genes mbili zinazokinzana na virusi. 

 Goodier, J., and Kazazian, H. (2008). "Retrotransposons Revisited: The Restraint and Rehabilitation of Parasites". Cell 135 (1): 23–35.doi:10.1016/j.cell.2008.09.022 . PMID 18854152

VVU-2 inadhaniwa kuruka kizuizi cha jamii au spishi katika angalau matukio matatu tofauti na kubadilika kuwa katika hali nyingine, hivyo kupelekea vikundi vitatu vya virusi hivi ambavyo ni M, N na O.

 Kalish ML, Wolfe ND, Ndongmo CD, McNicholl J, Robbins KE et al. (2005). "Central African hunters exposed to simian immunodeficiency virus". Emerg Infect Dis 11 (12): 1928–30. doi:10.3201/eid1112.050394 . PMC 3367631 .PMID 16485481

Kuna ushahidi kuwa wanadamu wanaoshughulikia nyama za mwituni kwa kuwinda au kuziuza, kwa kawaida hupata VSVU.Hata hivyo, virusi hivyo ni dhaifu na hukandamizwa na mfumo wa kingamwili baada ya wiki kadhaa za kuambukizwa. Inadhaniwa kuwa maambukizi kadhaa ya virusi hivyo kutoka kwa mtu hadi mwingine katika mfululizo wa haraka huhitajika ili vipate wakati unaotosha kubadilika na kuwa VVU.

 Zaidi ya hayo, kwa sababu ya kiwango chake kidogo cha kuambukiza kutoka kwa mtu hadi mwingine, virusi hivyo vinaweza tu kuenea katika wingi wa watu iwapo kuna njia moja au mbili za hatari ya kuambukizana ya kiwango cha juu. Njia hizi zinadhaniwa kutokuwepo barani Afrika kabla ya karne ya 20.

 Marx PA, Alcabes PG, Drucker E (2001). "Serial human passage of simian immunodeficiency virus by unsterile injections and the emergence of epidemic human immunodeficiency virus in Africa"Philos Trans R Soc Lond B Biol Sci 356 (1410): 911–20. doi:10.1098/rstb.2001.0867 .PMC 1088484 . PMID 11405938



Njia maalumu za hatari kubwa ya maambukizi zinazoruhusu virusi hivi kubadilika ili kuweza kuishi katika wanadamu na kuenea katika jamii yote hutegemea wakati uliopendekezwa wa kuvuka kutoka kwa mnyama hadi mwanadamu. Tafiti za kijeni za virusi hivi zinadokeza kuwa chanzo cha hivi karibuni zaidi cha VVU-1 ya kikundi M kilitokea mnamo 1910. Wanaotaja kipindi hicho maalumu huhusisha mzuko wa janga la VVU na kuibuka kwa ukoloni na ukuaji wa miji mikubwa ya kikoloni ya Afrika, huku ukisababisha mabadiliko ya jamii pamoja na kiwango kikubwa cha uasherati, uenezi wa ukahaba na matukio mengi ya vidonda vya viungo vya uzazi (kama vile kaswende) katika miji iliyochipuka.

 Worobey, Michael; Gemmel, Marlea; Teuwen, Dirk E.; Haselkorn, Tamara; Kunstman, Kevin; Bunce, Michael; Muyembe, Jean-Jacques; Kabongo, Jean-Marie M. et al. (2008). "Direct evidence of extensive diversity of HIV-1 in Kinshasa by 1960"Nature 455(7213): 661–4. doi:10.1038/nature07390 .PMID 18833279
  
. Miji ya kikoloni ya miaka ya kwanza ya 1900 ilijulikana kwa maambukizi ya viwango vya juu kutokana na ukahaba na vidonda vya viungo vya uzazi, hivi kwamba, kufikia mwaka 1928, 45% ya wanawake wakazi wa mashariki mwa Kinshasa walidhaniwa kuwa makahaba. Kufikia mwaka 1933, takriban 15% ya wakazi wote wa mji huo walikuwa wameambukizwa aina mojawapo ya kaswende.

 Sousa, João Dinis de; Müller, Viktor; Lemey, Philippe; Vandamme, Anne-Mieke; Vandamme, Anne-Mieke (2010). Martin, Darren P.. ed. "High GUD Incidence in the Early 20th Century Created a Particularly Permissive Time Window for the Origin and Initial Spread of Epidemic HIV Strains"PLoS ONE 5 (4): e9936. doi:10.1371/journal.pone.0009936 .PMC 2848574 . PMID 20376191 .
 
Maoni mengine yanadokeza kuwa hatua zisizo salama za uuguzi barani Afrika katika miaka ya baada ya Vita vya pili vya dunia, kama vile kutumia sindano moja tena na tena sindano zisizosafishwa kuchanja umati chanjo za magonjwa mbalimbali mfano chanjo za polio,tetanus nk, kuchoma dawa za antibayotiki na kampeni dhidi ya malaria ndizo njia za kwanza zilizoruhusu virusi hivyo  kuenea kutoka kwa mtu mmoja na kuambukiza wengine wanaotumia sindano iliyomchoma tayari mtu mwenye ugonjwa huu. na kupelekea kirusi hiki kubadilika mara kulingana na mazingira au mwili vinapoingia. .

 Marx PA, Alcabes PG, Drucker E (2001)."Serial human passage of simian immunodeficiency virus by unsterile injections and the emergence of epidemic human immunodeficiency virus in Africa"Philos Trans R Soc Lond B Biol Sci 356 (1410): 911–20. doi:10.1098/rstb.2001.0867 .PMC 1088484 . PMID 11405938 .

Chitnis, Amit; Rawls, Diana; Moore, Jim (2000). "Origin of HIV Type 1 in Colonial French Equatorial Africa?". AIDS Research and Human Retroviruses 16 (1): 5–8.doi:10.1089/088922200309548 .PMID 10628811

  
  
Visa vilivyonakiliwa vyema vya VVU katika mwanadamu ni vya mwaka 1959 katika eneo la nchi ya Kongo. Kuna uwezekano kuwa virusi hivyo vilikuwemo huko Marekani mwaka 1966,lakini maambukizi mengi yanayotokea nje ya Kusini kwa Sahara yanaweza kufuatiliwa hadi kwa mtu mmoja aliyeambukizwa na VVU katika nchi ya Haiti na kisha kuyapeleka maambukizi hayo nchini Marekani takriban mwaka 1969. Janga hili kisha lilienea kwa haraka katika vikundi vilivyo katika hatari kubwa ya kuambukizwa (mwanzoni ilikuwa ni wanaume waliofanya ngono na wanaume). Kufikia mwaka 1978, maambukizi ya VVU-1 katika mashoga wenyeji wa New York na San Francisco yalikadiriwa kuwa 5%, kuonyesha kuwa maelfu ya watu nchini Marekani tayari walikuwa wameambukizwa.

 Gilbert, M. Thomas P.; Rambaut, Andrew; Wlasiuk, Gabriela; Spira, Thomas J.; Pitchenik, Arthur E.; Worobey, Michael (November 20, 2007). "The emergence of HIV/AIDS in the Americas and beyond" (PDF). PNAS 104 (47): 18566–18570. doi:10.1073/pnas.0705329104PMID 17978186 

Hivyo baada ya kusema hayo niseme tu Yawezekana Ugonjwa huu ulikuwepo tokea zamani sana lakini umekuja kugundulika na kupewa Jina Miaka ya 1980. Na ile dhana kwamba ugonjwa Huu umetengenezwa na Richard Gallo si kweli bali yeye ni Mwanasayansi aliyefanya utafiti wa wagonjwa waliokua na Virusi hivi ndio akagundua shida zao za kiafya zinasababishwa na kirusi hiki na kukipa jina la HIV.