MWANASAYANSI wa Uingereza aliyekuwa akiishi Australia, Prof. David Goodall, ameaga dunia baada ya kujichoma sindano yenye sumu iliyochukua dakika moja kuchukua uhai wake.

Goodall mwenye miaka 104 alizaliwa jijini London Aprili mwaka 1914 ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza Vita ya Kwanza ya Dunia, na alikuwa mtaalam wa sayansi ya viumbe na maisha ya wanyama.  Alisafiri kutoka magharibi mwa Australia hadi Basel, Uswiss, kwa ajili ya kujitoa uhai kwa hiari, ingawa alisema anachukizwa na kitendo hicho.


Goodall amehitimisha safari yake ya mwisho akiwa amezungukwa na familia yake ambapo alishika bomba la sindano yenye sumu aina ya Sodium pentobarbital na kusukuma kwenye mwili wake, ambapo iliingia kwenye mishipa ya damu na sumu  ikaenea mwilini na kupoteza uhai wake.

Chakula chake cha mwisho kilikuwa ni samaki, chipsi na keki  huku akisikiliza wimbo wa Beethoven, Ninth Symphony.
Enzi za ujana wake.
Wakati wa pumzi yake ya mwisho, Goodall aligeuza kiti na kuruhusiwa kujichoma sindano hiyo ambapo kwa nchi kama Canada, Uholanzi, Luxembourg, Uswiss na sehemu nyingine za Marekani, sheria inaruhusu mtu kuamua kujiua kwa sababu maalum.
Akiagana na mjukuu wake.
Mwili wake utachomwa moto nchini Uswiss na kisha majivu kupelekwa Australia.