mofolojia fonolojia na sintaksia


Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya kwanza ni utangulizi, sehemu ya pili ni kiini cha kazi na sehemu ya tatu ni hitimisho la kazi kwa ujumla.

Sapir,(1921)ana fasili maana ya lugha kwa kusema "Lugha ni mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie kuwasilishia mawazo, maoni na mahitaji. Mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari" 

 Mgullu,R.S(1999) anasema "Lugha ni mfumo wa mawasiliano ya mwanadamu ambao hutumia mpangilio maalumu wa sauti kuunda vipashio vikubwa zaidi kwa mfano mofimu, maneno na sentensi" Pia anadai kuwa lugha ni mfumo wowote wa mawasiliano ya watu kwa mfano lugha ya Kifaransa. lugha ya Kihindi. 

Kamusi ya TUKI(1990)inasema,"Lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana" 

 Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo zimekubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika kukidhi mawasiliano yao ya kila siku katika nyanja mbalimbali za maisha mfano siasa, uchumi na utamaduni.


Semantiki ni taaluma katika isimu ambayo hushughulikia maana ya maumbo au sentensi katika lugha. Taaluma hii ilianza enzi za Aristotle na Plato ambao walizingatia zaidi sifa za maana, katika kipindi hicho walitaka kujua sifa na tabia za maana. Leech (1981).

Habwe na Karanja wakimnukuu Richard na Wenzake (1985) wanasema “Semantiki ni stadi ya maana. Semantiki ni utanzu unaochunguza maana katika lugha ya mwandamu”. Wanaendelea kusema semantiki hutafiti maana za fonimu, mofimu, maneno na tungo. Hivyo kutokana na fasili hii maana hushughulikiwa katika vitengo au viwango vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, mofolojia na sintaksia.

Hivyo  kwa ujumla  Semantiki ni taaluma katika isimu ambayo hushughulikia maana ya maumbo au sentensi katika lugha. Taaluma hii ilianza enzi za Aristotle na Plato ambao walizingatia zaidi sifa za maana, katika kipindi hicho walitaka kujua sifa na tabia za maana. Hii inamaanisha kwamba semantiki hutalii maana katika vipashio vyote vya kiisimu katika  viwango vyote vya lugha yaani fonolojia, mofolojia na sintakisia.

Semantiki kama taaluma nyingine ina mahusiano na taauma nyingine kama ifuatavyo katika mcoro na hatimaye katika maelezo yanayo eleza vipengele mbalimbali vya lugha:-
Mchoro kuonesha  mahusiano ya semantiki na vipengele vingine vya lugha kama sintaksia,mofolojia na fonolojia.Kuwepo kwa semantiki katikati inamaana kwamba tawi hili ni muhimili wa matawi mengine.

..






 Sintaksia, ni utanzu wa sarufi unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipasho vyake. Utanzu huu huchunguza sheria  au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ili yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika, . Kwa mantiki hii, kwa kuwa semantiki hushughulikia viwango vyote vya lugha, basi hushughulikia pia kiwango cha sintaksia ambapo huangalia maana za tungo, kwani tungo lazima ikubalike kwa wazungumzaji pia tungo lazima ilete maana.    
         Kwa mfano,
Pana huimba vizuri akiwa mubashara
Mubashara huimba vizuri akiwa pana.
Vizuri huimba pana akiwa mubashara.
Katika mifano hii sentensi (1) inampangilio sahihi katika lugha ya Kiswahili hivyo inamaana na inawezesha mawasiliano, na sentesi zilizobaki hazijafuata mpangilio sahihi wa kimuundo wa  lugha ya Kiswahili hivyo hazina maana na hazifanikishi mawasiliano. Hivyo semantiki ina uhusiano na mofolojia.
pragmatiki kuwa ni uchunguzi wa maana katika muktadha wa mazungumzo au maandishi na inavyofasiliwa na msikilizaji au msomaji. Semantiki na pragmatiki ni matawi yanayoshughulikia maana katika sentensi, semantiki inashughulikia maana za maneno na kuangalia muundo wa vipashio katika sentensi na pragmatiki inashughulikia maana inayohusisha muktadha. Pragmatiki inashughulikia maana isiyo ya msingi bali maana inayotokana na muktadha husika.
Mfano: neno baba katika muktadha wa kimapenzi ni mvulana wakati semantiki    
                    inashughulika na maana ya msingi ambayo inatoa fasili kulingana na kitu  
                    kinavyoonekana kwa mfano neno baba litafasiliwa kama ni mzazi wa kiume   
                    ambaye lazima awe na umri zaidi ya miaka kumi na naneMofolojia ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha katika kuunda maneno. Tawi hili la isimu huchunguzi na kuchambuzi wa maumbo ya maneno na jinsi maumbo hayo yanavyotumika katika lugha. Jukumu la neno husika katika sentensi hubainika vyema kulingana na uhusiano baina ya maneno mengine katika tungo. Maumbo ya kimofolojia huathiri vipengele vingine vya kisemantiki. Hivyo semantiki ina mahusiano na taaluma ya mofolojia kwa kuwa ili lugha iweze kueleweka lazima iwe na mpangilio na muundo mzuri wa vipashio vya sentensi ili kuleta maana katika mawasiliano.
Mfano:     Mwalimu anaimba
                     Walimu wanaimba
Katika mfano huu katika upande wa kiima kiambishi kinaashiria umoja na wa  inaashiri wingi,  katika upande wa kiarifu viambishi katika upande wa kiima vinaashiria nafsi yatatu umoja na wa vinaashiria nafsi ya tatu wingi, hivyo maumbo ya maneno lazima yawe na maana.
Pamoja na Semantiki kuangalia maana  ni dhahiri kuwa si taaluma pekee inayochunguza maana, kuna taaluma zingine zinazojitofautisha na Semantiki katika kuchunguza maana, miongoni mwa taaluma hizo ni,Semiolojia, Leksikolojia na Leksikografia.
Kuna wataalamu mbalimbali wanaofasili dhana ya leksikolojia kama kipengele kinachokaribiana na semantiki, baadhi yao ni;
 Ullmann (1962) ambaye anafasili leksikolojia kama ni tawi la isimu linaloshughulikia mofolojia na maana ya maneno.
 Doroszewksi (1973) kama alivyonukuliwa na Mdee (2010) amefafanua leksikolojia kuwa ni tawi la isimu linalochunguza etimolojia, maana na matumizi ya maneno. Hivyo basi leksikolojia ni tawi la isimu linalochunguza maana, mofolojia, etimolojia na matumizi ya maneno. Uhusiano wa semantiki na leksikolojia; taaluma zote zinashughulikia maana za maneno, leksikolojia inashughulikia maana zinazopatikana kwenye kamusi na mabadiliko ya maana za maneno kwa mfano neno mtoto maana msingi ni kiumbe anayezaliwa na binadamu na maana nyingine ni mpenzi na semantiki huangalia maana ya msingi kwa mfano neno mama ni mzazi wa kike.
Katika kuangalia dhana ya semiolojia Massamba (2004) amefasili semiolojia kama taaluma ya kisayansi inayojishughulisha na uchunguzi na uchanganuzi wa mifumo ya ishara mbalimbali ikiwa inazingatia zaidi uhusiano baina ya kiwakilishi na kitajwa.
 Ferdinand de Saussure kama alivyonukuliwa na Morris (1971) amefasili semiolojia ni uhusiano kati ya alama na kitu, jambo au hali ya kitu inavyowakilishwa, akaaendelea alama ni kiashiria na kitu ni kiashiriwa. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kiashiria na kiashiriwa.
 Charles (1934) alishughulikia dhana ya semiotiki kwa kuunda tanzu tatu ambazo ni sintaksia, Pragmatiki na semantiki. Sintaksia ni taaluma ya uhusiano kati ya ishara na vitu/ vielezo jinsi vinavyotumika, pragmatiki ni taaluma ya uhusiano kati ya mfumo wa ishara na mtumiaji wake na semantiki ni taaluma ya uhusiano kati ya maana na ishara. Hivyo basi semiotiki ni taaluma inayoshughulikia maana za ishara/ taswira.
 Semiotiki hushughulikia neno kama kiwakilishi (utajo) cha kile kitajwa pia hushughulikia maana ya msingi. Hivyo semiotiki inaona maana inapatikana kupitia taswira. Yaani kila taswira lazima inakuwa na maana inayowakilisha. Kwa mfano rangi nyekundu duniani inaashiria upendo hivyo maana ya upendo iliyojitokeza imetokana na taswira ya rangi hiyo
. Hivyo katika taaluma hii maana zote za maneno zimefumbatwa katika alama. Ni dhahiri kwamba ingawa semiolojia na semantiki hushughukia maana, semiolojia kwa kiasi kikubwa hujihusisha na alama za kitaswira na vielezo kwa kiasi kidogo wakati semantiki huchunguza maana katika mfumo wa ishara wa lugha inayozungumzwa na binadamu. Semantiki inatofautiana na semiolojia kwani semantiki inashughulikia alama za lugha yaani kila lugha huwa na alama zinazoashiria kitu fulani wakati alama za semiolojia hazihusu lugha yaani huwa ni maana za mawasiliano, mfano ishara za mawingu, wanyama kama bundi ishara ya uchawi.
 Vilevile katika kipengele hiki tunaona jinsi dhana ya leksikografia ilivyofafanulia, uhusiano na semantiki.
Mdee (2010) anafasili leksikografia ni kazi ya kisanaa na kisayansi ya kutunga kamusi ambayo hujumuisha uorodheshaji wa msamiati wa lugha inayotungiwa kamusi pamoja na maelezo yenye kufafanua kila neno lililoorodheshwa kadri ya mahitaji ya mtumiaji wa kamusi aliyelengwa. Semantiki na leksikografia huchambua maana na sifa za neno na uhusiano wa kimaana wa maneno yenye kuunda kikoa maana. Katika leksikografia maana za maneno zinapatikana katika fasili ya leksimu. Hivyo leksikografia huangalia maana inayopatikana kupitia fasili, pia taarifa mbalimbali zinazoingizwa katika kamusi kama za etimolojia, maana/fasili, matamshi, taarifa za matumizi humsaidia msomaji kupata maana ya leksimu.
Semantiki inahusiana na taaluma hizo kwani taaluma zote zimejikita katika kuangalia maana ya lugha, ingawa kila taaluma inaangalia maana hiyo kwa namna tofauti tofauti. Pia taaluma zote ni taaluma za lugha, hivyo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuonesha jinsi gani lugha inavyojiumbia maana kutokana na hali halisi iliyopo
Kwa ujumla semantiki ni tawi la isimu kama matawi wengine ya isimu ambalo haliwezi kujikamilisha lenyewe pasipo kuhusiana na matawi mengine ili kukamilisha mawasiliano. Lakini semantiki inaweza kutofautiana na matawi mengine kwa kuanza na tafsiri yake ambayo inajieleza na imetofautiana kabisa kidhima na matawi mengine ambayo ni fonolojia, sintaksia, na mofolojia. Pia dhima zake hazifanani na matawi mengine ya isimu.  Fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha, huchunguza jinsi ambayo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha ya mawasiliano. Ili lugha ya mawasiliano iwe kamili ni dhahiri kwamba mpangilio wa sauti lazima uwe na maana ili kufikisha ujumbe, hivyo semantiki inauhusiano mkubwa na fonolojia.
Mfano: Neno “UA” linamaanisha sehemu ya mmea pana maalumu kwa kutoa mbegu na kuvutia wadudu kwa ajili ya uchavushaji lakini ikibadiliswa vitamkwa na kuwa ‘au’ huleta maana tofauti na maana ya  awali.

                                                   MAREJEO
Habwe, J na P. Karanja (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.
Massamba P. B. D (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI

Massamba, D.P.B na wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo.          Dar essalaam: TUKI.
Richmond H Thomason (2012). What is semantics? Second version. Oxford press

Massamba (2004) anafasili dhana ya semantiki kuwa ni taaluma ya isimu inayojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa maana za maneno na tungo katika lugha.

Mgullu,R.S(1999)Mtalaa wa Isimu,Fonetiki,Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili, Nairobi Kenya, Longhorn Publishers.